Ni Video ikimuonyesha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo akikabidhiwa Fimbo ya ushindi pamoja na Kuku aina ya Jogoo na wazee maarufu Baada ya kuwatembelea katika kukagua uhai wa chama hicho sambamba na kuhamasisha vijana kushiriki katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Tukio hilo limetokea katika kata ya Shiloleli iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Geita ambapo wazee hao wamefunguka nini Maana ya kukabidhi Fimbo hiyo ambayo ni mwongozo katika shughuli mbalimbali za kichama zinazofanywa na kiongozi huyo.