Wazee muhimu wasife na kuicha CCM peke yake

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wazee muhimu ninamaanisha wazee wenye akili nyingi, wenye hekima na wanaoifahamu vema Tanzania. Wazee hawa ni wale wote wenye hadhi ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Kikwete, Mzee Warioba, Butiku, Cleopa Msuya, Malecela, Msekwa, Karume, na wengine wa aina hii.

Kule Marekani na Ulaya wazee wazee wao wa aina hii kama vile George Washington na wengine kabla ya kufa walihakikisha kuwa wanaacha checks and balance za kisiasa kwenye mataifa yao kwa kuacha vyama zaidi ya kimoja vyenye nguvu sawa na katiba imara ili viwasaidie wananchi wao baada ya wao watakapokuwa hawapo tena duniani. Waliacha dira za mataifa yao na vyama na taasisi imara zitakazoshindana kwenye kuitekeleza dira yao wakati wao hawapo duniani tena.

Mwalimu Nyerere ilikuwa anaifahamu siri hii ya mataifa ya ulaya na Marekani, lakini alishindwa kuitekeleza yote kwa 100% kutokana na waliokuwa wanamzunguuka kushindwa kumuelewa kabisa, alijaribu lakini hakufua dafu. Mwl. Nyerere alifahamu kuwa baada ya yeye kufariki dunia ile checks and balance aliyokuwa ikiifanya yeye haitakuwepo kabisa kutokana na hurka na ufahamu wa watu waliokuwa wakimzunguuka. Hii ndiyo sababu iliyomsukuma Baba wa Taifa kukubali na kulazimisha Tanzania ikubali mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 ingawa wenzake walimpinga. Yeye alitaka kuwepo na vyama 2 vya siasa vyenye nguvu sawa ili vikosoane kwenye masuala ya nchi. Yaani vishindane hoja na sera katika kuitawala nchi, chama kimoja kikizembea na kuboronga chama cha pili kinarekebisha kama inavyotokea Marekani, Uingereza na nchi nyingine za ulaya.

Nyerere aliwafahamu sana watu wake na CCM yake, alifajua tu kuwa akiondoka yeye CCM itatunga sheria na kanuni za Kikaburu za kuumiza watu bila kujali, watakuwa madalili wa mali za wananchi, watajilimbikizia mali na madaraka bila kuhojiwa na wataendelea kubaki madarakani kwa nguvu za dola. Na kweli sasa hivi CCM haitegemei kupiga kampeni tu ili kushinda chaguzi, zipo sheria na taratibu kwaajili ya kuibakisha CCM madarakani sio kwa manufaa ya watanzania na wana CCM bali kwaajili ya viongozi na familia zao. Leo hii nafasi zote nzuri za ajira na uongozi zimejaa watoto wa viongozi na jamaa zao zao.

Hata wanaCCM walio wengi wanatoka kapa, wanaambulia t-shirts na kofia na posho wakti wa kampeni baaaasi.

Wazee wetu hawa muhimu kama wataondoka duniani na kuviacha vyama vya upinzani vyootenchini vimekufa au havina nguvu kabisa wajue kuwa wameliacha taifa lisokuwa na matumaini, watakuwa wameiacha Tanzania kwenye njia mbaya kabisa kuwahi kutokea. Wameliacha taifa bila ya mtu wala taasisi yoyote inayoweza kuhoji chochote kizuri au kibaya kama wanavyohoji akina Mzee Butiku na Warioba wakati mwingine. Kila atakayehoji kitu kibaya atatungiwa sheria ya kumthibiti kama walivyokuwa wakifanya makaburu. Taifa litaanza upya kutafuta uhuru na demokrasia kwa njia ngumu sana.

Nitoe wito kwa hawa wazee waone mbele kama wezao akina washington na Nyerere kuhusu mataifa yao. Wasiangalie matumbo yao ya kizee eti kwasababu watoto wao pia wamejumuishwa kwenye ulaji. Ulaji wa aina hii haudumu na sisalama kwa taifa, sio kwamba watu wote (raia na askari) wataendelea kuangalia hali hii iendelee milele.
 
Mtoa mada...hao wotee wamejaa utajiri wa kutupa,na wamekula mema ya nchi kweli kweli.mimi hapa duniani naskitika mtu masikini kufa maana hajala mema ya nchi...kwanini afe kabla hajaonja vitamu? Uliowataja hata wakienda Jerusalem sawa tu.!!
 
Umeandika vizuri sana. Ila hao wazee uliowataja katika vipindi vyao nao walikuwa hovyoo hovyoo tuu..kama jk na msuyaa.. kidogo kina warioba waliofanya kazi na mwalimu. Cha msingi hapo ni kwamba nchi hii haiwez kombolewa na mikono ya hao wazee uchwara bali ni jukumu la wananchi wenyewe kuikomboa nchi yao!
 
Mbaya zaidi wamebaki wachache Sana, na vijana wa ccm wa kufuata nyayo zao siwaoni, wamebaki vijana mapambio , ila sio mbaya ccm Haipo na siku zake zipo Chache Sana itafutika sio mda
 
Orodha yao wote iko kwenye mioyo ya wananchi, kundi ambalo linapokezana na watoto na kisha wajukuu wao kupata maisha nafuu kupitia utawala wa nchi. Mwl. Nyerere hakukipenda kitu hiki hata kidogo, na ndiyo maana watoto na wajukuu zake hakuwaingiza kwa makusudi kwenye mnyororo wa nchi, hakuupenda usulutani wa ukoo mzima kuwemo kwenye serikali milele. Alitaka mtoto wake aingie kwenye siasa kwa utashi wake na merit.
 
Upo sahihi kabisa
 
Mbaya zaidi wamebaki wachache Sana, na vijana wa ccm wa kufuata nyayo zao siwaoni, wamebaki vijana mapambio , ila sio mbaya ccm Haipo na siku zake zipo Chache Sana itafutika sio mda
Hiyo ndiyo mbaya zaidi, watoto wao wanaobaki hawana haiba kama ile ya wazazi wao, hivyo wanashindwa kujenga hoja za kuwaaminisha na kuwashawishi hata wana wanaCCM wenzao waendelee kuimba iyena iyena hata hata pale wanapokuwa na hali ngumu kimaisha na nchi inapokuwa inaporwa. Hata kwenye mikutano ya siasa hawaendi hadi wapewe chochote. Vijana wao watabaki madarakani kwa kutunga sheria kandamizi za kikaburu, na huu ndio utakaokuwa mwisho wao.
 
Umeandika vizuri sana. Ila hao wazee uliowataja katika vipindi vyao nao walikuwa hovyoo hovyoo tuu..kama jk na msuyaa.. kidogo kina warioba waliofanya kazi na mwalimu. Cha msingi hapo ni kwamba nchi hii haiwez kombolewa na mikono ya hao wazee uchwara bali ni jukumu la wananchi wenyewe kuikomboa nchi yao!
Nimeskitika sana mtoa mada kumtaja mzee wa msoga
 
Yani watu walio haribu nchi,ndo tuwategemee kuisaidia tena nchi!!!!!!!
 
Hakuna wazee hapo ni matapeli tupu
Wazee hawa wanafahamu sana kuwa baada ya wao kuondoka duniani hakutakuwa na atakaehishimiwa, aminiwa, kuthaminiwa wala kusikilizwa sio tu na wanchi bali hata ndani ya wanaCCM wenyewe. Ikifikia hapo taharuki ya kutunga sheria kandamizi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola vitaongezeka nchini. Hii itawaunganisha watanzania wengi dhidi ya kitabaka hiki nufaika cha kinasaba.

Ni heri wazee hawa sasa, leoleo wasaidie kuimarisha demokrasia nchini ili watu wasiopenda sera za chama kinachotawala watumie vyama vilivyoratibiwa kupinga badala ya kutumia vikundi na njia ambazo sio rasmi. Hivi ndivyo wanavyofanya Democrats na Republican, Labour Party na Conservative, etc. Na Mwl. Nyerere alikusudia hivyo yatokee Tanzania baada ya yeye mkosoaji mkuu atakapokuwa hayupo duniani lakini Wenzake hawakumuelewa kabisa. Nyerere alikerwa na utitiri wa vyama bali alitaka vyama vikubwa 2 tu vikosoane vinapofanya uzembe kwa wananchi. CCM haikubali kukosolewa na haina mkosoaji kwasasa, wazee wote muhimu wana conflict of interests na serikali maana watoto wao wamepewa ulaji na watawala ili kuwanyamazisha. Vyama vya upinzani navyo vimekabwa kooni ile mbaya kwa sheria za kikaburu na matumizi mambaya ya vyombo vya dola dhidi yao.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema kaburu ni kaburu tu bila kujali ngozi yake. Kuhahakikisha kuwa vyama vya siasa na viongozi wake hawafurukuti hakuna tofauti na yale yaliyotokea kwa ANC dhidi ya National Party cha makaburu, tofauti ni kwamba wale walikuwa weupe na hawa ni weusi.
 
Ilitakiwa faida ya uwepo wao tuione sasa lakini kwa bahati mbaya hatuioni,
 
Back
Top Bottom