Wazee muhimu wasife na kuicha CCM peke yake

Uwepo wao unamsaada Gani kwa Nchi sindio hao wanataka Katiba ibadilike ili watoto wao waendelee kugawana mamlaka hao wazee wako ni Hasara kwa Nchi

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Umeeleza vizuri, hawa wazee ni matapeli tu bora wafe wote tuanze upya
 
Jibu ni kupanua wigo wa siasa katika nchi. Akili nzuri sana zipo hata nje ya CCM, ukizifunga pingu nchi itadidimia. Na hili ndilo hao unaowaita wazee wa CCM wamekuwa wakijaribu kulifanya katika uhai wao wote. Sishabikii kufa kwao, lakini Mwenyeezi Mungu ndio mjuzi katika kuiletea nuru Tanzania au na Wazee hao au bila wazee hao.

Kimsingi tunatakiwa tufikirie nje ya box, kwani pale walipotufikisha hatutatoboa kama hatutalitoboa box.
 
Hakuna watu wa ajabu kama hao wazee walio wahi kushika madaraka nchi hii,wanajiona mungu mtu, kwamba wao na family zao ndio wanauwezo wakuongoza nchi,ndo sababu wakifa watu wanashangiria na kubeza
 
Wazee hawa hawana haya hata kidogo. Kwanza wanashangaa kuona eti vyama vilivyoleta uhuru kule Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, nk vyote havipo madarakani leo hii, Wanaviona wajinga kushindwa na wapinzani. Miundombinu ileile tuliyoitumia kupambana na makaburu na wareno kuzisaidia nchi za kusini mwa Afrika kudai uhuru wao sasa hivi ndio inatumika kuvikandamiza vyama vya upinzani visinyanyue shingo.

Hata hivyo, Nadhani hata sisi wananchi ni majuha sana, unyumbu wetu wanautumia kikamilifu.
 
Hakuna watu wa ajabu kama hao wazee walio wahi kushika madaraka nchi hii,wanajiona mungu mtu, kwamba wao na family zao ndio wanauwezo wakuongoza nchi,ndo sababu wakifa watu wanashangiria na kubeza
Iko siku kama sio wao wenyewe basi watoto au wajukuu zao hawataamini kile watakachokiona, itawatokea kama ndoto usingizini. Watakujakuambiwa kila kitu wanachokijua leo kuwa ni chakwao na kumiliki kumbe sio chao ni cha serikali. Wananchi watagawana hata suti na bakuli zao. Historia na ukweli havina tabia ya kupotea. Kuna mtu anateuliwa kuwa DC na mbunge mpaka askari wanajisikia kichefuchefu kumpigia salute. Iko siku udhalilishaji huu pia utawachosha,
 
Ubinadamu wetu unatutaka kufa. Ipo siku watakufa. Matumaini ya Taifa letu hayako mikononi mwa wanadamu tuache kuchuliana. Na wala sio lazima kila mzee anabeba vision ya umoja na ustawi wa Taifa hili. Wengine wako kimaslahi zaidi
 
La Kikwete naye yumo?
Nimeishiwa hata nguvu za kusoma mpaka mwisho.
Mzee kikwete ni miongoni mwa wazee wanaokwenda sana mataifa ya wengine kama Ulaya na Marekani ambako vyama vya upinzani ndio kimbilio la wananchi na taifa. Mfano, bila kuweko kwa democrat imara wamarekani ingewawia vigumu kuondokana na Trump. Wanafahamu uzuri wa kuwa na vyama vingi vikubwa lakini wamekaa kimya wakati vyama vya upinzani vinanyamazishwa kwa hila.
 
Huyuhuyu aliyeuza dhahabu yetu tukipewa vyandarua? Aliuza gesi yetu.
Kina Bush, Obama, Clinton,walikuwa wanapishana Dar utafikiri ni Texas.
 
Nani kakudanganya nchi ni chama au wazee.
KILA zama na kitabu chake
 
Huyuhuyu aliyeuza dhahabu yetu tukipewa vyandarua? Aliuza gesi yetu.
Kina Bush, Obama, Clinton,walikuwa wanapishana Dar utafikiri ni Texas.
Haha, alitaka kuwauzia Kigamboni yooooote. Eti mji wa kisasa.
 
Watu wazima wote hata watoto wanaojielewa wapiganie nchi yao iwe salama kwa wote kuishi.
Hizi fikra tegemezi ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
 
Watu wazima wote hata watoto wanaojielewa wapiganie nchi yao iwe salama kwa wote kuishi.
Hizi fikra tegemezi ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
Sio fikra tegemezi ila ni namna bora ya ku manage planed change. Vijana wao waliowaachia wamepoteza uwezo wa kushawishi badala yake wanatumia nguvu kufanikisha kila kitu
 
Sio fikra tegemezi ila ni namna bora ya ku manage planed change. Vijana wao waliowaachia wamepoteza uwezo wa kushawishi badala yake wanatumia nguvu kufanikisha kila kitu
Hao wazee tuwaache wapumzike na washauri wakiweza.
Watu wenye nguvu ya kimwili na kiakili wawajibike kulinda taifa.
We must have a competent succession plan.
 
Mwalimu alifanya kosa kubwa kutubadilishia kipande tu cha Katiba ili kuruhusu siasa ya vyama vingi... Kwa kweli mabadiliko haya yameghalimu maisha ya watanzania wengi mno hadi muda huu - mfumo huu umefanya watu kufa, kufilisiwa, kufungwa, kunyanyashwa nk

Mwalimu angetupatia katiba mpya kabla ya kughatuka, kwa kweli katuachia mzigo mkubwa mno kiasi cha kuligawa Taifa letu makundi mawili - wanaotaka mfumo wa mwaka 1977 ambao chama tawala ndicho kinachoshika hatamu ya uongozi mia kwa mia na wale wanaotaka mfumo wa kidemokrasia, taasisi za kutoa haki kuwa huru bila kuingiliwa na watawala.

Bado tupo katika giza nene, Mwalimu umetuachia mzigo mzito mno.
 
Ukikumbuka yaliyotokea Zanzibar katika uchaguzi wa Mwaka 1995, namna ambavyo CUF wali-perform, nashindwa kukubaliana na wewe juu ya Nyerere na dhamira ya dhati ya mfumo wa vyama vingi.

Kaunda aliyekubali kushindwa, waiona nchi yake ikibadilisha vyama bila bughudha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…