Wazee na wakubwa zetu mtatisha sana mkifanya mambo yafuatayo;

Wazee na wakubwa zetu mtatisha sana mkifanya mambo yafuatayo;

Opulent

Member
Joined
Sep 6, 2024
Posts
33
Reaction score
40
Katika ukuaji wetu wanadamu tunakua na ndoto na matamanio mbali mbali kama gari ya ndoto, nyumba ya ndoto etc, hata kama tupo kwenye hatua ambayo haikupi harufu yakuweza yafikia mambo Yale uyawazayo lakini ndoto na matamanio hua yapo, na hivyo katika utafutaji wetu tunakua na taswira mbali mbali zijazo mioyo yetu, na changamoto mbali mbali tutamanizo kuondokana nazo pindi tupatapo uwezo na rasilimali.

Sisi hatuna uwezo wakufanya maamuzi nakufanya mambo yatokee kama ninyi mlivyo na uwezo na ni ngumu kujishughulisha na changamoto zisizo wagusa moja kwa moja kwani mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Kuna kujisahau pakubwa sana kule ulikotoka na jinsi ulivyounga unga maisha hatimae neema na kudra za mwenyezi Mungu kukuzukia nakukuketisha mahali pajuu.

Tumesikia wito na mahimizo yenu ya sisi kujiajiri kama mnavyotuambia kila siku tujiajiri na tunapambana kufa kupona ikiwezekana kesho tuje tuwalee kama wazazi wetu. Sisi Wala hatuhitaji kuleta ushindani kwenye position zenu ila ushindani juu yenu nasi mnaufungulia pale ambapo mnashindwa kuhakikisha tunakua occupied kule mnakotusukumia.

Kabla sijaendelea naomba tuwe na hizi tafakuri mbili:

1. Kwanini ni ngumu kuingiza pesa kwenye uchumi wa Taifa letu? Kwa nini Paypal na miundo mbinu mingine muhimu ya malipo itambulikayo nakuaminiwa duniani haifanyi kazi?

2. Kwanini ni rahisi kutoa pesa kwenye uchumi wa nchi zetu nakupeleka kwenye chumi za nchi za nje?

Kwa namna nyingine swali hilo juu laweza kua Kwa nini Amazon, Alibaba etc zinafanya kazi vizuri kabisa Ina maana wazee wetu mlipata changamoto kipindi cha nyuma hata ikawa kipaumbele chenu kuhakikisha haya majukwaa yanafanya kazi mtakapopata mamlaka ya maamuzi?

Turejee kichwa chetu kisemavyo, Wazee na wakubwa zetu mtatisha sana mkifanya mambo yafuatayo;

1. Mkiufungua uchumi wetu nakuungamanisha na dunia hasa kwenye zama hizi za gig economy.
Vijana wengi sana tumejiongeza nakujiajiri baada yakusaka ajira huku na kule bila mafanikio hatimae kuikubali wito wenu wakututaka tujiajiri, Hapa nawasemea vijana wale waliojichanganya na dunia Kisha kujiajiri kwenye gig economy kama Mobile and website developers, Drop shipping, graphics designing, voice over artists etc. Changamoto kubwa Katika kundi hili ni miundo mbinu ya malipo duniani mfano PayPal kutofanya kazi kwa wakazi wa Tz, huko duniani M-pesa zetu hazijulikani mwajiri atakuambia nipatie your PayPal details usemapo PayPal haifanyi kazi huku nilipo ndio deal umelikosa hilo wakati mwingine kazi imeshafanyika ila ndio hivyo malipo huyapati despite kuwekeza nguvu na rasilimali muda wako kwenye kazi husika. Wizara ya fedha tusilale kwenye hili mtatisha sana mkilifanya hili jambo kua history Kuna vijana wengi waliacha nakwenda kuuza matunda barabarani na mitumba karume despite kua wamesoma ila maumivu yakushindwa kupata ujira au kukosa deal kisa mifumo ya malipo kidunia haifanyi kazi.

2. Venture capital funding eco-sytem(Ufadhili wa mtaji wa ubia)
Hivi karibuni tumeona Nia ya mama kusupport startups akaanzisha mfuko kuwezesha vijana kujikwamua kiuchumi maarufu kama pesa za Mama Samia, Pesa za mama zimekutana na leakage zakutosha kulingana nakutokua na good systems in place mchakato mzima umegubikwa na unprofessionalism kiasi kwamba ni rahisi watu Fulani fulani wasio hata na biashara kujipatia fedha ambazo zilizokusudiwa ziende kwenye biashara, Tujiulize nchi za wenzetu wanafanyaje kuwawezesha vijana?

Nchi za wenzetu Kuna venture capital funding Kwa startups and small business - Ufadhili wa mtaji wa ubia (venture capital) ni aina ya uwekezaji wa fedha unaotolewa na wawekezaji kwa kampuni changa au biashara ndogo ndogo ambazo zinaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kukua. Wawekezaji wa mtaji wa ubia kikawaida huwekeza fedha zao kwa kubadilishana na umiliki wa sehemu ya hisa katika kampuni hiyo. Fedha hizo mara nyingi hutumika kukuza shughuli za kampuni, kuendeleza bidhaa mpya, au kuingia kwenye masoko mapya. Badala ya Serikali kudeploy mitaji hii Kwa maelfu ya watu kwenye vikundi, ni kheri hizi pesa tungewapa hata watalaamu wa venture capitalist hata kama watakua ni wa kukodi watusaidie kudeploy kwenye startups zenye potential yakukua nakuajiri maelfu ya watanzania, Marehemu Rughe Mutahaba former boss wa clouds aliwahi sema "hakuna tajiri ya kikundi bali Kuna tajiri mmoja mmoja" mchakato huu Ungekua wazi kwakurusha hata vipindi vya pitch sessions kwenye runinga ili vijana wapate access yakujifunza namna yakunavigate kwenye issue zakuraise capital hivi ndivyo tunaweza kutengeneza efficiency na uelewa wa haya mambo Kwa vijana. Venture capital system ya iliyopo Kwa sasa ni venture seminar sio venture capital Vijana wamejazwa kwenye incubators mwanzo mwisho kupewa seminars na madalali watakao kuraise grant funding Toka Kwa wafadhali huku wakiwatumia vijana kama stepping stone kutibu njaa zao.

Mwaka 2023 startups za majirani zetu Kenya ziliraise zaidi ya $550 million from venture funding huku sisi tukirakse $20 million. Figures zinaongea zenyewe kua Iko shida mahala.

3. Futa baadhi ya kozi mavyuoni zisizo na tija nakuwekeza nguvu kwenye hard skills zitazomsaidia kijana kuikabili mitaa.

Ndio tunasema mtu achague kile atachoenda kukisomea kadri moyo wake upendavyo lakini haiondoi ukweli ni kwamba still vijana tunahitaji msaada wenu, we are still too young to make bad choices yatayogharimu kesho yetu chukulia kijana anaenda kusomea bachelor ya mambo ya archaeology and artifacts Sijui aje avumbue fuvu lipi tena, Mnaweza tusaidia kwakuondoa machaguo ya kozi yasiyo na tija yanayopelekea paralysis in decision making.

4. Kama tunataka kwenye list ya top ten wazawa matajiri waonekane in ten to twenty years basi hatuna budi kuwaexpose vijana wetu na mazingira ya nje kwenye nchi zilizoendelea.

Exposure ni kitu muhimu ambacho wazawa wengi tunakikosa mfano mfanya biashara wa Dar akienda mkoani kufanya biashara hatokua sawa na yule wa Mkoa husika, atakua na vitu vya ziada vitavyompa competitive edge. Ukichunguza Kwa ukaribu startups za vijana wakitz zinazo fanikiwa kuraise funding ni zile za vijana wenye exposure na mazingira ya nje mfano Benjamin Fernandez wa Nala, Usiri brothers wa Ramani, Elia Timotheo wa East African Fruits, wote hawa vijana startup zao zimeraise billion Tshs in funding, Wana exposure ya nje(Wamesoma nje).

Pia ukiangalia wakongwe kina Mengi na Kina Ali Mufuruki wote hawa walisoma nje na Wana exposure nzuri juu ya mifumo ya ubepari na namna ifanyavyo kazi. Hata hawa wa Asia waliopo Top watoto wao wamesoma nje na ndio waliosaidia hata kuscale Kwa kampuni zao, Ni vyema kwa serikali yetu kuendelea kutoa scholarships hata kwa nafasi 10 kwa watz hasa kwenye fani za Computer science na Biashara watakaosoma nakurejea kujenga nchi.

5. Kuwa makini sana na haya makampuni makubwa kama Voda.
Makampuni haya mengi yatoka enzi za baba zetu yameendelea kuenjoy huge margins kwakutaka yafanye kila kitu menyewe, muda mwingine yame lobby against washindani, mfano mzuri ni Kushindikana kupatikana Kwa huduma ya star link kwakigezo Cha Ofisi ili hali nchi jirani zime embrace mabadiliko ambazo tungeweza hata kuigilizia kwao. vijana pia wamepoteza startups zao kwa cartels kampuni kama hizi.
**************"
 
Back
Top Bottom