Wazee tukumbuke.!!

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Mwimbaji Hassan Rehani Bitchuka. Bendi siijui.
Bomu limeshapasuka,
Walanguzi wanahangaika
Mhujumu nayo iko ndani eeh.

Nilikuwa Mimi silali
Nikihangaikaika na mawazo
Nikifikiria maisha
Kwangu yalikuwa magumu eeh.

Nilikuwa na wake wawili
Mmoja nimeshamuacha
Sababu ya matatizo
Maisha yalipanda ooh.
Eeeh maisha magumu eeeeh.

Nikilala nikiamka,sukari haionekani
Nikilala nikiamka unga hauonekani
Nikilala nikiamka , sabuni haionekani.
Sababu ya hai walanguzi eeeh.

Sasa Vita imetangazwa jama,wananchi wote tuwe imara. Vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi ooh×2

NB .Kila zama Ina wahujumu wake,
Vijana mjikaze tu safari ni hatua,tumetoka mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…