Shining Light
JF-Expert Member
- Jan 8, 2024
- 406
- 523
Wengi tukikutana na connection fasta tunapaparuka kutaka kuiona, wengine tukitaka kuhakikisha kuwa ni kweli au kusuuza macho tu, utafikiri inaongeza chochote kwenye maisha yako!
Hivi unajua siku mwamba akakusnich na kukuripoti unambaza connection ndio umekwisha?
Kuna matatu, ni ama ulipe faini ya milioni 20, uende jela miaka 7 au upigwe spana zote mbili, yaani uende jela na faini ulipe.
Sasa kwa maisha haya ya kibongo kibongo laki tu mtu inakutoa jasho kwenye milioni 20 hiyo tunajua 99% hatutoboi, ni jela moja kwa moja.
Kama huwezi sambaza connection ya dada yako, mama yako, baba yako au kaka yako kwanini uwe mwepesi kusambaza za wengine?
Kuwa muungwana kwa kuwa mfano bora kwa wengine uwapo mtandaoni.
Nakukumbusha tu: Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 ni kosa Kisheria Kusambambaza Picha za Mnato (still pictures) na Picha Mjongeo (Video) zinazoashiria vitendo vya Ngono au Utupu
Ukikutwa na hatia, adhabu ni;
1. Faini ya Milioni 20
2. Kifungo jela Miaka 7
3 Au vyote kwa Pamoja