Chief-Mkwawa Kwanini Google stadia ilifail wakati naona ilikuwa na potential kwa sababu ulihitaji tu kuwa ni kifaa cha interneet kama tv na chrome cast, laptop basi.
Hahikuhitaji ununue game consoles za bei mbaya na mtu unaweza kucheza game kali kali maana computing power inafanyika kwenye cloud.
Lakini mwisho ikafail na kufungwa. Ni kwanini?
Stadia hata haikua best kwa Hilo wote Microsoft na Nvidia walikua na service ambazo ni superior.
1. Microsoft ana Xbox Gamepass ambayo ukilipia unapata Games bure kwenye Pc yako, Games bure kwenye Xbox yako na games bure Online kwenye kustream, watu wengi wana Either Xbox ama pc, kwanini ununue stadia? Hasa vile Games za Xbox ni kali na sio vigemu vya simu.
2. Nvidia ana Geforce now ambayo kama umeshanunua game unaweza kulistream bure. Atleast kwa wakati huo.
3. Kuna Streaming platform nyengine kama Moonlight (Sunshine) ambazo una self host mwenyewe.
Gamers wengi ni rahisi kwenda kwa Microsoft ama Nvidia badala ya Google sababu Games kali zote zipo huko.
Changamoto nyengine ambayo imazikumba platform zote hizi ni ping, unahitaji kuwa na server karibu mno kustream games.
Assume Unacheza Fifa mpira unaanza unatoa pasi, ukibonyeza X kwenye pad ina maana data zinatoka kwenye pad hadi stadia, stadia inazi upload kwenye internet yako kama Zuku, Zuku ina peleka waya za Baharini, ziende hadi Marekani huko, server ilete feedback hadi Tanzania tena kabonyeza X ndio uone mabadiliko kwenye tv ya ile pasi, is it possible? Ngumu sana. Inahitaji server iwe hapa hapa Dar kuenjoy games za kustream.
So kutokana na ping issues watu wachache ndio walipata experience nzuri na kama unavyomjua Google ikala panga.