Wazee wa klabu ya Simba wamuomba Rais kumpeleka CAG kukagua klabu hiyo

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ampeleke CAG kupitia na kuikagua Klabu ya Simba ikiwemo kupitia sheria kandamizi na za kibaguzi katika michezo.

Wazee hao wameonesha kutokubaliana na Mkutano mkuu wa Klabu hiyo Jumapili unaotarajiwa kufanya mabadiliko ya katiba wakidai mkutano huo ni batili kwani viongozi wa klabu hiyo wamekwisha ibadili katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama kuipitisha tu kinyume na sheria inavyowataka kuunda rasimu kwanza na wanachama waisome watoe mawazo yao ili ipitishwe na kuwa Katiba.

Wazee hao Wamepinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi wanataka itambulike Katiba ya mwaka 2014.

Chanzo: ITV
 
CAG si ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali?! Kama jibu ni ndio basi Aden Rage alikuwa sahihi kuhusu hawa jamaa.
 
simba naitabiria kama yanga. siasa siasa siasa
 
CAG si ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali?! Kama jibu ni ndio basi Aden Rage alikuwa sahihi kuhusu hawa jamaa.
Ni kweli wa serikali lakini pia kwa OMBI maalumu anaweza kwenda kukagua popote pale kwenye maslahi ya umma...refer case ya Chama cha Walimu.
 
Yaani unaweza kuzeeka ila ukabaki na makapi kichwani, Sasa mkaguzi wa hesabu za serikali na Ukaguzi wa Kilabu wapi na wapi, kuna mizee inakera hata kwa mawazo yao.
 
Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ampeleke CAG kupitia na kuikagua Klabu ya Simba ikiwemo kupitia sheria kandamizi na za kibaguzi katika michezo.

Wazee hao wameonesha kutokubaliana na Mkutano mkuu wa Klabu hiyo Jumapili unaotarajiwa kufanya mabadiliko ya katiba wakidai mkutano huo ni batili kwani viongozi wa klabu hiyo wamekwisha ibadili katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama kuipitisha tu kinyume na sheria inavyowataka kuunda rasimu kwanza na wanachama waisome watoe mawazo yao ili ipitishwe na kuwa Katiba.

Wazee hao Wamepinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi wanataka itambulike Katiba ya mwaka 2014.

Chanzo: ITV

Nawaheshimu sana wazee wangu, ila hivi vizee vya Simba na Yanga ni hasara kwa Taifa. Leo hii Yanga inapata shida kwasababu ya vizee kama Akilimali. Pumbavu!!
 
wanajuwa mianya ya kula imefungwa. Simba hakuna wazee wala nini hii ni club ya wanachama wasituletee mambo ya kizamani mpira ni biashara sisi washabiki muhimu ushindi tu. Hawa wanajiita wazee ni lazima wafungwe midomo wote na hata wale wa Yanga maana ndio wanarudisha hizi club nyuma wao kuamini mpira ni uchawi tu. Team zote mbili hizi lazima ziondokane na fikra za hawa wazee. Mpira wetu utakuwa siku team hizi zikiwa katia ushindani ulio sawa sio mmoja yuko vizuri mwingine njaa Yanga akija shiba njaa inahamia kwingine. Tunataka team zote mbili katika ubora bila migogoro hapo mpira wetu utakuwa.
 
Hao wazee wakae kwao wasikilize mpira redioni huku wakinywa ghahawa. Mambo yamebadilika, this is modern football, wasikariri miaka ya 50s huko.

Wakae watulie, watu tunatoka katika zama za ubabaishaji tunaingia kwenye modern management systems. Walizowea kula kwa dezo
 
Yani hizi klabu simba na yanga ni shida sana , timu iko vizur wanataka kuivuruga tena wazeee ni nani ! hawa ndio wanaufanya mpira wetu usiendelee , warudi kijijin wakalime jaman mianya ya kupiga pesa hamna
 
Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ampeleke CAG kupitia na kuikagua Klabu ya Simba ikiwemo kupitia sheria kandamizi na za kibaguzi katika michezo.

Wazee hao wameonesha kutokubaliana na Mkutano mkuu wa Klabu hiyo Jumapili unaotarajiwa kufanya mabadiliko ya katiba wakidai mkutano huo ni batili kwani viongozi wa klabu hiyo wamekwisha ibadili katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama kuipitisha tu kinyume na sheria inavyowataka kuunda rasimu kwanza na wanachama waisome watoe mawazo yao ili ipitishwe na kuwa Katiba.

Wazee hao Wamepinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi wanataka itambulike Katiba ya mwaka 2014.

Chanzo: ITV
Hawa wazee nyambaffu zao sana, timu inafanya vizuri na tumekuwa wamoja, wanataka kuanza kumwaga sumu!
Hawa wazee wa Simba na Yanga ndio WACHAWI wa soka la bongo!!
Wakalee wajukuu zao, zama zao zimepita.
 
Hawa wazee sijui wapoje timu ikisimama tu kidogo wanaanza tu mambo zao mfyuuu
Hawa wanatumiwa na upande wa pili mitulinga sc
Kwnz hawataki mabadiliko wakati wakiachiwa timu hata sku moja hawana hata mia ya kuendesha
 
Back
Top Bottom