Wazee wa mambo hadharani kesho tena wanaingia uwanjani kutoa burudani

Wazee wa mambo hadharani kesho tena wanaingia uwanjani kutoa burudani

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Timu ya Yanga kesho itatupa karata ya pili katika mashindano ya Mpumalanga cup kwa kucheza dhidi ya TX Galaxy.

Mechi itakuwa live Azam sport 1 HD saa kumi jioni. Mechi ya Yanga ya kesho itahitimisha mashindano ya Mpumalanga kisha itahamia kwenye mashindano ya Toyota Cup tarehe 28 kwa kukipiga dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mechi zote za Yanga zitaoneshwa live mambo hadharani sio siri siri kama mko jandoni.
 
Ni bora Yanga inawatendea haki mashabiki zake wapate burudani mubashara kabla ya msimu kuanza. Wanaona kikosi chao kilivyo, namna ya uchezaji wao, ubora wao, n.k. maana wenzetu wanasubiri wafanyiwe surprise kwenye kilele chao.
 
Wengine mechi zao za siri na wanacheza na vitimu vya dajara la chini huku wakijiita timu kubwa wakati inafanya mambo kijanja janja. Wameshindwa kufuvunja mkataba wa mchezaji kisa mil 600. Alafu wanajitokeza na kusema wao timu kubwa sijuwi ukubwa wa wapi.
 
Back
Top Bottom