Wazee wa "road trip" safari yako ilikuaje 2021/22?

fabinyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
3,042
Reaction score
2,221
Yangu/yetu ilikuwa poa sana.

1. Ilianzia 07 Dec 21 alafajiri sana kwa kutoka Namanga via Arusha, Kilimanjaro, Pwani to DSM (was so smooth)
2. Baada ya wiki hivi asbh saa nne j2 fulani baada ya chai nikaenda Dodoma via Chalinze/Moro (hii inilipa kero kutoboa Moro maana malori mengi,buses,mara misafara ya viongozi 😬)
3. Baada ya siku mbili nikanyoosha goti kwenda Tarime kutokea Dom,Via Singida Nzega, Shy-Mwigumbi, Maswa, Bariadi, Lamadi then Tarime (was smooth ride,niliianza sa tisa hivi usiku maana ni safari ndefu,almost kms 800,ukimaliza unaskilizia tako,kiuno na mikono😀)
4. Then baada ya xmas,nikaingia Musoma mjini kwa siku mbili tatu( haka katrip kapo soft)
5. Then nikaenda Mwanza kutoka Msm (soft trip) na nilala Bunda usiku mmoja.
6. Nikamalizia Mwanza (baada ya kupokea mwaka na kukaa wiki hivi) to Arusha via Shy,Singida,Babati ( Hii trip nzito niliianza alfajiri sana,ila muda karibu wote wa asbh uliliwa na ukungu mzito hivyo kutembea kama bibi harusi, na kipande cha road Mwz - Shy nikibovu,usipokua makini unavunja miguu)

All in all safari kama alivyoshaauri Rrondo katika uzi wake ambao nimeunakili title
1. Uwe na gari zuri lenye uwezo (langu no B lkn bado linauwezo mzuri na comfo ya kutosha, cc 2000 vvti)
2. Kampani nzuri nzuri (nlikuwa na familia,mke na watoto wadogo wanne,jenga picha hapo safari ilikuwaje😀)
3. Mfuko lzm uwe vzr kwa kweli ( kama 3 mil hivi imekata,tutatafuta ingine)
4. Jumla ya Kms nilizokata kwa mzunguko wote ni 3,506....nyingi ni kwenye lami na kama kms 100 zilikuwa ni rough road)

Ushauri zaidi kama unataka trip yako iwe nzuri,ongeza haya
1. Kwa safari ndefu, lala mapema na uanze safari asbh sana...tisa,kumi sio mbaya kwa mwili unakua na nguvu. Mpk jua linatoka uko mbali. Usinywe pombe kabla ya kulala na wakati wa safari.
2. Weka vituo vya kupumzika hasa wakati wa kunywa chai,lunch,kuchimba dawa,kupiga picha etc. Kama ukiset vzr,utatumia muda huo kuonana/salimiana na ndugu na jamaa kama wapo ktk miji utakayopita, ni kitu kizuri sana. Hakuna haja ya mpera mpera mwanzo mwisho kama umepanda bus,relux furahia safari kama vipi lala kabisa katika miji midogo. Pia unaweza kupiga kamoja,safiii..
3. Usishindane mbio na madereva wengine, tena wasaidie wakuovatake,haina maana kabisa...nimeshuhudia ajali 2,moja nissan wingroad na IST 😃,Mungu jalia hapakua na vifo ila gari zimeharibika vibaya na safari inakuwa ishakufa hapo. Kuwa na speed muafaka,binafsi nilikuwa sizidi 120 na umakini wa hali ya juu
4.Fuata alama za barabarani,zinasaidia mnooo maisha yako hasa kwa barabara ngeni na kuepusha migongano na askari wetu. Aidha Askari wa barabarani wengine sio wa baya kama tujuavyo,kikubwa ni kuomba radhi pale penye makosa. Na ukiwa na familia wanakuelewa haraka sana hivyo faini huzipati.
5. Service muhimu sana kila baada ya kms kadhaa hasa unapomaliza trip fulani, mbali ya kufungua boneti na kuangalia ya humo, ingiza gari shimoni kagua hata kama husikii shida yoyote...trust me gari inapotembea some nuts,bolts hufunguka,vitu kukatika nk..... Kagua sana tairi, studs na hasa upepo (nashauri kila baada ya km 300).....upepo huongezeka kutokana na msuguano na kupelekea tairi kupasuka na kusababisha majanga makubwa .
6. Be suspicious, jua harufu, sauti na kila kitu cha gari lako, itakusaidia kuepusha hatari nyingi na uharibifu wa chombo. (Kuna wkt kuanzia speed 100 hivi, nikifunga break, naskia sauti ngeni. Kumbe tairi moja ya mbele wkt nafanya service fulani walitoa tairi,katika kurudishia ni stud mbili 2 tu ndio zilifunga na kubana vzr,3 walilazimisha kufunga kumbe hazijakaa ktk njia zake, hvyo licha ya wao kufunga na kuona zimetaiti kumbe hazikufika mwisho🙄)
7. All in all,muombe sana Mungu kabla ya safari na mjikabithi kwake mda wote, hili la kuzingatia sana.

So far, The trip was sooooo gud...seeing nature when traveling is amaizing....na jana tarehe 05 Jan 22 ndio nimeingia Ar...Naamini kuna jambo utajifunza na litakusaidia. Ofkoz,mimi husafiri mara kwa kwa mara kwani ni kitu nachokipenda hasa self drive. Asanteni Mwanza kwa kuupokelea mwaka mpya hapo, Mwz kutamu sana kwa kweli.

Trip yako ilikuaje?Kms ngapi umemaliza?ulienda wapi na wapi?Please,share nasi tujifunze hata kama ulipata majanga, pole lknsisi tutapata somo,
Asanteni

NB. Kuwa na plan ya trip yako na anza maandalizi mapema, make money kdg kdg naamini utafanikiwa.
😬
 

Hongera brother,
Mimi nilitumia Masaa 18 Bukoba to Dsm
Nimetoka saa 12 kasoro asubuhi nimeingia dsm saa Sita na nusu usiku
Speed 120 to 140 KM/hr napunguza mwendo kwenye TUTA na yale Mashimo na viraka vya bararani.
Mpaka nafika dsm nimepigwa TOCHI mara SABA.
Gari ilikuwa TOYOTA ALLION 1.8 L na ilibeba mzigo wa kutosha hivyo ikawa stable barabarani.
 
Aisee umenitamanisha Sana yaani Kwa kifupi safari ukiwa na familia ina Raha yake hasa ukienda salama na ukarudi salama....
2019 December nikifanya safari Tamu kama hiyo dar - mwanza - bunda- kisorya- ukerewe
Alooo,safi sana Mkuu,family is the best company ever.....so kirorya pale uliipandisha kwa kivuko?kidogo sana niende UK,nikaambiwa na watoto kwenda kule naweza kulogwa,nikaacha 😀
 
Dah,kama nakuona...hiyo trip ni ndefu haswa,zaidi ya km 1300...ulikaza sana,hongera sana.
 
Bila shaka hii gari yako ni ipsum/picnic.

Hii gari ni nzuri sana kwa familia aisee ina legroom ya kutosha hata mtu mrefu anakaa bila shida yoyote..

Kwa wenye familia kubwa hii gari inafaa sana
 
Ulipiga full tank Ngapi?
 
Mkuu Arusha_ Mwanza ulitumia muda gan?
 
Dom to Nyasa, Gari Baby Walker Toyota Raum, safari kuanza saa kumi na moja kuingia Songea saa kumi na moja, tukalala kesho yake Songea to Nyasa our final destination, nilikuwa mm na shemeji yenu wawili tu, nilienjoy sababu ni kama nilikuwa nafanya utalii wa ndani vile, kuna sehemu ukipita unavuta true oxygen Mungu aliyokusudia tuvute binadamu hewa safiiiiiii mpk mapafu yanashituka[emoji23]..!!!, Hakika kusafiri ni tiba.
 
Mimi nilitoka Dom to mwaza hadi tarime. Siku ya kwenda nili enjoy japo nilipata shida ya kukamatwa na traffic hadi kufikia kuwekwa mahabusu,(nilichukulia changamoto za kawaida kama nyingine tu), nilifika hadi sirari. Kurudi pia nilienjoy sana nilitoka tarime jioni nikaenda nikalala Mwanza kesho yake nikatoka mwanza saa nne saa mbili nipo Dodoma
 

Ulipita njia ipi?nilishwahi kwenda Mbinga,kupitia Iringa,wkt wa kurudi nikapitia Lindi…was amazing..Kweli kusafiri ni tiba na shule…hongera sana
 

Duh,mahabusu tena?[emoji3]we utakuwa Mtata sana mutu ya tarime
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…