Tetesi: Wazee wa Tanga wamemsusa Yanga Omary

Tetesi: Wazee wa Tanga wamemsusa Yanga Omary

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Takribani mwezi mmoja na ushee umepita tangu Yanga Omary awekwe ndichi.

Kama ilivyo ada ya wazee wa Tanga na vitongoji vyake kijana wa mji anapopatwa na matatizo bila kujali ameyaita mwenyewe au yamemfuata yenyewe, huwa wanakaa na kufanya dua,kisomo au tambiko maalumu kwa ajili ya kuwaomba miungu wamfanyie mhusika wepesi katika matatizo yake.

But kwa hili la Yanga Omary wazee wanaonekana kumsusa.

Wazee Magwiji na.mafundi wa jijini Tanga karibu wote wamemkaushia Yanga Omary kama hawamjui vile. Hakuna kisomo,dua wala tambiko.

" Yule bwana mdogo mwache ajifunze ili akili zimkae sawa. Kwanza alikuwa na kibri kwa watu na hakuwa na ushirikiano mzuri na wazee" Anasema mmoja kati ya wazee magwiji wa jijini Tanga.

"Kama angekuwa anaishi na watu vizuri sisi wenyewe tungefanya kufru bila hata yeye au nduguze kutuomba" Anaendelea mzee huyo.

Kama wewe ni " kijana wa mji" unatakiwa kuishi vizuri na wazee.
 
Kwani Nini kimemkuta Yanga Omari???hiyo mambo ya ndichi mimi binafsi sijaelwa! Tujulishe mkuu nini kimemkuta huyo Jamaaa???
 
Ameingai ANGA za kamishna Jenero wa nani lii.. Akakutwa na Usage Usioruhusu hata kupewa Dhamana na Mahakama
 
Back
Top Bottom