Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
Wazee wa Yanga waliongea na vyombo vya habari jana na kumshambulia Mengi kuwa aache kumkashifu mfadhili wao bwana Yusuph Manji. Walisema mambo mengi sana ila kubwa ni kuwa Mengi aachane na Manji kwa kile ambacho wanajaribu kuonesha kuwa Mengi anamwonea wivu. Kwamba amwache kabisa mfadhili wa Yanga. Je, wanaelewa kinachoendelea au wanajali vijisenti wanavyoimbiwa na baadaye kupewa kupitia mlango wa nyuma kwa kivuli cha ufadhili? Je wanauchukia ufisadi au kwao nchi kuibiwa si neno ili mradi wamepewa pilau na biriani?