Ukiwanyima wananchi wako elimu , watakuwa watumwa wa kila kitu.Elimu ya darasa la saba haitoshi na ndio chimbuko la umasikini wetu na mawazo ya kipuuzi na kipumbavu kama ya hawa wazee.
natamani mabomu ya mbagala yangetua vichwani mwa mafisadi.
Hawa ni watumwa wa gredi ya chini wanaohongwa allowance, kahawa na kashata.
Wapo wale watumwa wa gredi ya juu wanaohongwa magari, nyumba, trip za majuu, nk. Hawa wanamadigrii, maPhD na wanashikilia ofisi za juu serikalini. Wakistaafu wengi wao wataishia kuwa kama hawa hawa watumwa wa gredi ya chini.
Wote hapo juu naona mmekaa Kisimba simba ngoja tuwasubili wana jangwani wenyewe tuone msimamo wao na wao wanasema kuhusu hili...
Waacheni jamani, angalau wakati tunasubiri hatima yao kupitia kwa YAN GA tunarejeshewa hela zetu kiaina kwa kuinua michezo. GT yupo? au bado amelala?
Mimi ni mwana Yanga, lakini natanguliza utaifa mbele, hao wazee ni watumwa waacheni na utumwa wao, itachukua mda kuwaelimisha nini kinaendelea katika nchi hii, hivyo waacheni wafu wawazike wafu wao
Hii naona ndio suala la kubeba njaa kwenye mfuko wa nailoni (transparent)! Hawajui hata wanachotetea ni nini! Kumbukumbu kubwa iko tu pale wanapoitwa Quality plaza kwa mazungumzo na bahasha, baada ya hapo watatetea kila uozo regardless....ovyo....
Mkuu kama ungesikiliza chanel 10 hawa wazee wameongea maswala ya busara wanasema kama Mengi anaushahidi kuhusu Mfadhili wetu Manji kuwa ni fisadi papa basi afuate utaratibu wa kufikisha malalamiko yake yaani aende polisi au TAKUKURU au ampleke mahakamani wanadai Mengi yeye si hakimu wa kukaa na kumnyoshea mtu kidole wewe fisadi papa wewe fisadi dagaa.
Pundamilia07;438784]Mkuu Fidel Mimi nadhani sehemu kubwa ya wachangiaji wanapofikia kujadili hoja fulani hawaangalii substance ya hoja zilizofikishwa kwao.
Mkuu Fidel
Mimi nadhani sehemu kubwa ya wachangiaji wanapofikia kujadili hoja fulani hawaangalii substance ya hoja zilizofikishwa kwao.
Kama watasoma au kusikiliza kwa kwa makini hawa wazee wanaowaponda hapa ni kwamba waliamua kutoa taarifa yao hiyo baada ya kutafakari kuwa utaratibu na sheria hazikungatiwa na Mengi wakati anafanya press conference yake. Kwa maana ya kuwa hakutowa ushahidi na vielelezo juu ya tuhuma zake. Na kikubwa kabisa ambacho wazee wale wa Yanga (ambao wengine wanawaita hawakusoma) wameonesha busara yao hata ya kuonesha nini Mengi angefanya, yaani kufikisha ushahidi na vielelezo vyake katika vyombo husika. Sasa kwa wale ambao wanataka kuwa hukumu hawa wazee kwa kueleza misimamo yao kama klabu wanakosea kwani klabu ya Yanga ina mahusiano na Manji kama mfadhili wao.
Nadhani ni vema tukaagalia uzito wa hoja ya wazee na sio kuwakashifu kwa maneno ya kejeli, hatujengi na hatuwatendei haki.