Wazee wa Yanga wanamtetea Manji!

Mtoa hoja ndio kachanganya na title yake ya kiunazi, wazee wamemchalukia Mengi. Wazee wamesema taratibu za kisheria zifuatwe kwa sababu nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria kama Manji anamakosa basi Mengi akamfungulie mashtaka kwenye vyombo husika.

Kuwatukana wazee wa watu kwa sababu ya kumbeba Mengi sio poa na ni lazima watu wawe na mawazo tofauti na yenu. Mengi kachemka kama anavyochemka mara nyingine, media yake anaitumia vibaya na victims ni wengi tu.

Vita ya ufisadi, Kabila na dini sio sababu ya kumfanya awe na haki kuliko raia wengine. Hata Mengi anatumia njaa za watanzania kuwarubuni pia, wahariri wa IPP media wasingekuwa na njaa wasingetumia airtime na space kumpamba kila kukicha. Kesho mtamsikia anatishiwa kuuawa acheni kulazimisha watu wengine waamini mnachoamini nyie.
 
Jamani kwa wadau mnaokumbuka Mengi alivyoitafuna NBC miaka ya 80 (kama inavyosemwa na baadhi ya watu" tunaomba tuelezwe ilikuaje wengine hatufahamu kilichojiri kwenye sakata hilo. Plz kama kuna mwenye data amwage tunazisubiri ili tuweze kupima usafi wa bw. Mengi!
 
Nawasikitikia saana watanzania wenzangu!mnakaribisha ukabila kwa nguvu..... Mnakuja katika udini kwa nguvuuuu zaidi mungu atunusuru na awanusuru pia akili na mawazo potofu mlioanza kuwa nayo.
Wazee wetu wametoa tamko la busara kuwa mbaguzi mengi hana haki ya kumhukumu yeyote bali aweche utawala wa sheria ufanye kazi utatamkaje masuala ya jeetu patel ili hali tayari yupo chini ya uangalizi wa dola? Yeye analo la kujibu katika kesi yake ya nbc? Kiwanja alichouzia kwa kampuni fulani...?ili hali aliomba serikali kwa ajili ya kujenga orphans? Kweli nyani haoni kundule nie mwacheni aendele ku-organizer tuzo za wanasiasa bora na kama alivyojitahidi kuifanikisha ya bi.kilango. Lakini asiwache kuandika katika this day kuhusu kiwanja cha milambo /samora lakini mhusika anajuwa nini mengi anataka na alichokikosa kwa rostam,manji,malima,masha na masilingi atakipata anachokitafuta muda si mrefu mnanishangaza mnaojifanya eti ni yanga mwana yanga hawezi kuwa mpumbavu siku zote wanajangwani ni watu wenye busara ndio maana tuna wazee wenye kila aina ya heshima na taahdhima
 
Kama kuna maneno mazito niliyowahi kuyasoma ni hayo ulosema mkulu.
Tupo pamoja.
 

Mkendanchi,
Huwa ninakawaida nikiona posting iliyo chini ya kiwango inanijibu huwa siipatilizi kabisa. Lakini vilevile huwa ninangalia pia kama mtu anayejibu huenda anahitaji kuelimishwa au kukumbushwa masuala muhimu.
Sitakujibu maswali yako 1 hadi 6, kwani ni kuingilia huru wa klabu ya Yanga ambao sote inabidi tuuheshimu kwa kuzingatia Yanga ni taasisi kubwa kongwe ambayo imekuwepo na kupata mafanikio mengi kupitia kwenye busara za wazee wake ambao wewe unawaona si kitu mbele ya macho yako.

Ninachotaka kufanya hapa ni kukukumbusha kuwa walichofanya wazee wa Yanga ni kutoa misimamo yao kama wazee wa klabu ya Yanga ambayo ina mahusiano ya moja kwa moja na Manji. Zaidi ya hapo wakaelekeza kama Mengi anajambo lolote lenye ushahidi basi afikishe kwenye mamlaka husika. Sasa Mpendanchi, kuongea maneno yenye busara kama haya unahitaji kuwa na PhD ya Havard au kuwa na shibe ya mapesa ya haramu?

Tuwaunge mkono wale wote wanaoelekeza mema, ninamaanisha wanaolekeza kufuatwa na kuzingatiwa sheria
 
Mzee Kenyata enzi zake aliwaita watu kama hawa wazee wa Yanga "malambaji ******". Wazee wa Yanga wameingia mtego kama CCM! Chama tawala kilipoanza kufadhiliwa na matajiri (na mafisadi wamo) ndio ukawa mwanzo wa kuwa "bubu" linapokuja swala la ufisadi. Tumeona juzi na jana jinsi Waziri Sophia Simba alivyokimbilia kuwatetea watruhumiwa wa ufisadi papa kana kwamba wao ni wanyonge hawana uwezo wa kujisemea! Jibu ni rahisi. Mama Simba alikuwa anarudisha fadhila kwa Tani Somaiya kwa kufadhili uchaguzi wa UV-CCM kwa kiasi cha Milioni 400 za Tanzania. Yanga isipoangalia itabandikwa timu ya "Fisadi Papa".
 
Pundamilia,
kuonesha kuwa wewe ndiye upo chini ya kiwango ndiyo maana huna majibu ya hayo maswali, kwani ungekuwa na kiwango ungetafakari kidogo ukipata majibu yake utajua tu hao wazee hawakwenda kwa niaba ya yanga wala siyo kwa masilahi ya yanga bali ni masilahi ya FISADI Manji
 
Join Date: Sun Aug 2008
Posts: 57
Thanks: 0
Thanked 8 Times in 7 Posts
Rep Power: 21
Join Date: Tue Mar 2009
Posts: 31
Thanks: 10
Thanked 17 Times in 12 Posts
Rep Power: 0
Join Date: Tue Nov 2007
Posts: 122
Thanks: 53
Thanked 56 Times in 37 Posts
Rep Power: 22


Mwaka huu kazi ipo kweli kweli. Sina hakika kama wote tunamjua na tunapambana na adui mmoja.
 

Bado ninaamini kuwa wewe unahitaji kuelimishwa tu.

Kwanza, kwangu mimi kuweka posting ya mtu chini ya kiwango haimaanishi hiyo posting ipo chini ya kiwango kwa mtu mwingine. Kuweza kuiweka katika kiwango cha chini inategemea na vigezo vyangu ninavyovitumia na wala haviwezi kuwa sawa na vya mtu mwingine.

Pili, si kila posting utakayokuwa umeiweka hapa basi ni bora kwa kila mtu, la hasha, kwani kila mtu ana uwezo wake wa ku-make judgement kwa vile anavyosoma.

Tatu, ni kweli na ninarudia kuwa sina majibu ya maswali yako kwani maswali yale yanajibiwa na mamlaka husika za wanayanga na siyo mtu yeyote. Ninakushauri maswali yako yaelekeze kwa viongozi na wazee wa Yanga, kwa kukusaidia, kama wewe ni mwanachama wa Yanga, basi kuna taratibu unaweza kuzifuata kwa mujibu wa katiba ya Yanga.
Labda mwisho nikuulize swali la kizushi, unapoita press conference kuna gharama gani unazotakiwa kuingia?
 
Uliwaona Ze komedi week iliyopita wao wako grade gani? Wale wazee njaa hasa Mzimba alipika kalele weeeeeeeeee.....akaja akapewa trip ya kuzunguka nchini na viposho kimya ataongea akiwa na shida anaenda kuvua mshiko teh teh...hapa wanataka swala la Ufisadi lipelekwe kwenye U-simba na U-Yanga.
 
Njaa mbaya sana inaweza kukufanya umsahau baba yako!
 
Hii nchi bora tuchapane kidogo nadhani heshima itarejea. Upuuzi umezidi kila kona.
 
Heheheeh count me out.....misaada hii wakati mingine ni mitego!


Masa,

Una bahati kwamba wewe unayaona hayo! Watu wengi wameingia mkenge na jinsi mambo yanavyokwenda tutaanza mchakato wa kuwatangaza watakatifu Manji, RA na mafisadi wenzao wakingali hapa bongo! Watampiku hata Nyerere kwani kila mtu sasa anaimba usafi wao. Naomba basi mimi niitwe fisadi ili hawa jamaa waachwe kuitwa mapapa!
 
Matukio katika vilabu vikubwa Simba na Yanga nadhani yanajieleza, kwa hiyo hatuhitaji sana kuumiza kichwa kuhusu hao wazee. Mchana kutwa huwa wanakaa kwenye vijiwe vya kahawa kujadili mambo yasiyo na maana, na jioni ni lazima ajaribu kutafuta sehemu ya kuchonganisha ili apate cha kurudi nacho nyumbani, ndio maana utaona migogoro haiishi.Manji kawashika hao wazee na akafanikiwa kumaliza mgogoro wa lile tabaka la Mzimba kwa kuwapa fedha na pilau, and that's all matters to them. Kwa hiyo watatetea chochote kile asemacho Manji kwa kuwa ndio wanaishi kwa staili hiyo. Haieleweki timu kama Yanga na Simba zinaendelea kuendeshwa kwa mtindo wa kizamani wa kutembeza bakuli wakati wanahazina ya mashabiki nchi nzima. Mabadiliko yoyote hayawezi kuwafurahisha hao wazee, bahati mbaya hata vijana nao huwa wamo katika hilo. Tunachoweza kwa sasa ni kuwapuuza na kupambana na huu ufisadi mpaka mwisho. Manji siyo mjinga wa kutoa fedha tu, alitegemea siku itafika support itakapohitajika, na wazee hawakumwangusha. What a shame!!!
 
Wazee hawa ,kama Mengi, wamejiingiza kwenye mainstream politics ambazo zinagusa hisia za Taifa zima.
Mtu anayekuibia ,tahadhari ukipewa ni jambo muhimu sana.
Hata Mwalimu wakati fulani, wakati wa ukombozi wa Rhodesia (Zimbabwe) na Afrika Kusini aliwahi kusema hawa wakubwa (Marekani na Uingereza)hatuwawezi kwa kuwapeleka mahakamani au kwa kuwazuia, kilichobaki ni kuwazomea na kuwapigia kelele.
Kelele za maskini ni muhimu sana katika siasa.
Africa Association (baadaye Yanga iliasisiwa nayo)ya wakati huo walifanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuwahasasisha umma juu ya uhuru wa Tanganyika.
Leo Mengi alichokifanya ni hivyo hivyo. Watanzania tunaibiwa na watu walio na ubia na wanasiasa leo unataka ushahidi.Utaupata wapi?
Kinachotushangaza wengi ni hawa wazee kukosahekima ya kuienzi Yanga kama klabu yenye historia nzito nchini
 
sasa hii inahusianaje na mpira maana hizi njaa zitatuua
 
Kweli hii nchi sasa haina mwenyewe ni mahame...upo wapi mwalimu weee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…