Wazee wenzangu wa huduma za kifedha na biashara nyinginezo hua mnashughulika vipi na aina hii ya wateja?

Wazee wenzangu wa huduma za kifedha na biashara nyinginezo hua mnashughulika vipi na aina hii ya wateja?

Shozylin

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
341
Reaction score
699
Yeye: habari.

Mimi: Salama karibu

Yeye : Asante huku aangaza nje ya mabango yaliyo nje ya milango, nakuuliza M-pesa ipo au hakuna.

Mimi: ipo unataka ku...?

Yeye: Aah sawa ili atoe 15,000 inabidi awe na sh ngap?
Mimi: Awe na 16,500

Yeye: Namba ya wakala ni iko wapi huku anapiga smu akitaka kutajia mteja?
Mimi: nikamuuliza yeye anae toa yupo wapi?

Yeye; yupo ( .....) Anataja wilaya nyingine ndani ya mkoa tuliopo.
Mimi: Natafakari nikamuuliza kwanini Asikutumie wewe pesa ili wewe ndo uotoe?

Yeye: Shii, hayo ni maswali ya ziada, ivi wewe unafanya kazi au hufanyi kazi, nikakaa kimya nikikuamcha amalize kuongea. Kama hufanyi kazi sema niende kwingine.

Mimi: Basi sawa we nenda kwingine tu ukahudumiwe.

Wazee wenzangu wa biashara hizi za kifedha na iana zozote biashara hua mna solve vip mnapo kutana na wateja wa aina hii.

NB: hua hairuhusiwi kutuma au kutoa pesa kwa mteja alipo mbali.
 
Mteja kutoa pesa nje na eneo lako akiamua kukufanyia uhuni anaweza, atatoa alafu atapiga simu kuwa amekosea kutoa. Mtandao husika wakiangalia mnara wataona ni kweli kutokana na umbali, pesa inaweza kurudishwa kimyakimya au wakakupigia simu. Bahati mbaya usipokee simu, pesa itarudishwa.
Mweleweshe mteja kuwa hairuhusiwi kutoa pesa mtu akiwa mbali, japo wateja ni wabishi.
Wateja wengine huona akikataa wakala huyu nitaenda kwa mwingine, hilo tu anaweza kuongea anavyotaka.
Usiwe na maneno mengi, ukiona hajakuelewa mpe ruhusa aende.
 
Back
Top Bottom