kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,521
- 2,747
Kama mnavyojua kesho tar 06/04 /2018 kuna mapambano makali ya kukata nashoka kwenye uwanja wa kinesi, binafsi nasubiria kwa hamu pambano kati ya Mada Maugo Jr aka mbunge mtarajiwa wa Rorya na Kanda Kabongo, utamu wa pambano hili ni kuwa Kanda Kabongo kaomba marudio baada ya pambano la kwanza kulambishwa sakafu mara kadhaa, pia mmoja wa walimu wa Kanda Kabongo ni Japhet Kaseba ambaye nae ameshachapwa vibaya na Mada Maugo, lingine ni kati ya Boniface Mwakyembe na Dulla Mbabe, lingine litakalokuwa na ushindani ni kati ya Mfaume Mfaume na Habibu Pengo hili litakuwa na mkanda.
Kesho ndio kesho wazee wenzangu wa ndondi njooni tutoe maoni yetu.
Kesho ndio kesho wazee wenzangu wa ndondi njooni tutoe maoni yetu.