Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WAZEE WETU HAWAKUWA NA PENSION, WALITEGEMEA KILIMO NA UFUGAJI; SISI ITAKUWAJE?
Anaandika, Robert Heriel.
Zamani ilisemwa; Jembe halimtumpi Mkulima, ikimaanisha kuwa Ukilima lazima uambulie chochote kitu. Iwe ni masikini au tajiri lazima upate. Hii ilitokana na Hali nzuri ya tabia ya nchi, mvua, jotoridi, jua, Ardhi yenye Rutuba n.k. Lakini Kwa sasa msemo huo pengine unapoteza maana Kwa Zama za sasa, jembe siku hizi laweza sio tuu kumtupa Mkulima Bali hata kumuangamiza kabisa.
Mabadiliko ya tabia ya nchi, ongezeko la kutisha la watu, ni moja ya majanga yanayokabili ulimwengu Kwa sasa.
Mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri Kwa kiwango kikubwa Sekta ya kilimo na Ufugaji. Uhaba WA mvua, na mvua zisizotabirika, ukame, kiwango kibovu cha unyevunyevu angani(humidity), baridi Kali imekifanya kilimo kuwa kigumu Kwa Wakulima wa chini ambao Kwa nchi zetu ndio wengi.
Mabadiliko hayo yatafanya Kilimo kiwe cha matajiri tuu wenye mitaji ya kutumia mifumo ya umwagiliaji, Teknolojia za kisasa, mbegu Bora, viwatilifu sahihi, na pembejeo zingine za Kilimo pamoja na uwezo wa Kulipia gharama za manunuzi ya Ardhi na kulipia Kodi.
Kilimo kilisaidia Wazee wetu Kupunguza gharama za maisha Yao Kwa kuwa na akiba ya chakula walau Gunia kadhaa zilizowasaidia mpaka Mwaka mzima. Huku mifugo nayo ikitumika Kama mboga au chanzo cha Mapato ambayo ilisaidia mahitaji madogo madogo Kama mboga, nguo, marekebisho ya Makazi na kukabiliana na changamoto za kifamilia.
Wazee wetu wengi hawakuwa wameajiriwa hivyo wengi hawakuwa na Pension, Kilimo na ufugaji ndivyo viliwasaidia kukabiliana na maisha wakati WA Uzee wao.
Sasa Sisi ndio Vijana, walipopitia Wazee wetu ni njia hiihii tuliyopitia ingawaje tofauti yetu na wao ni vyombo tulivyotumia. Wao walitumia Farasi na Punda, Sisi tunatumia Magari na Ndege.
Ni hakika wengi wetu hatutaajiriwa, wengi wetu uzee wetu hautakuwa na Pension wala Mafao. Je tumejipangaje?
Kama ni kilimo na ufugaji nimeshaeleza hali halisi hapo juu.
Kama ni biashara, wote tunafahamu ni ngumu Sana kui-maintain biashara Kwa miaka ishirini mfululizo. Wachache Sana hufanikiwa katika hili. Je tumejipangaje?
Itakuwaje?
Wazee wetu mbali na shughuli za kiuchumi Kama Kilimo na ufugaji Kama sio uvuvi. Lakini pia Taasisi Kama ya ndoa zao zilikuwa thabiti Kwa kiwango kikubwa.
Familia zilikuwa na nguvu kutokana na wazazi Baba na Mama kuhakikisha familia inakuwa pamoja kivyovyote mpaka mwisho. Hiyo ilipelekea kusaidiana kimajukumu.
Wanawake walilima, walichunga ng'ombe na iujishughulisha na shughuli za kiuchumi Kama walivyo Wanaume. Kwa lengo la kujenga familia na sio ubinafsi.
Lakini Sisi Zama hizi, familia zetu hatuna uhakika kama zitadumu mpaka kwenye umri wetu WA Uzee, tukisaidiana Kama Wanandoa. itakuwaje?
Taikon huwaga nasema, Ugumu unaoupata kuiunganisha familia yako ndio itakuwa kitanzi wakati WA uzee wako.
Kadiri Unavyoshindwa kuiunganisha familia, kuleta umoja na ushirikiano ndani ya familia yako ndivyo unavyofanya uzee wako kuwa Mgumu Sana. Kwani watoto nao hawatakuwa na umoja na ushirikiano.
Wamama wanaovunja ndoa bila sababu za maana, wanaobeba majukumu na kuvunja Haki za Baba ndani ya Familia Uzee wao nao ni hakika utakuwa Mgumu.
Tumaini la Masikini lipo Kwa Watoto wake. Ndio maana nimeingiza Hoja ya Familia.
Shughuli uzifanyazo pekee hazitoshi kukupa Nafasi nzuri nyakati za uzee. Isipokuwa na namna unavyoijenga Familia yako.
Kusomesha pekee watoto haitoshi,
Bali watoto wanapaswa uwafundishe upendo, umoja na ushirikiano wao Kwa wao, kuheshimiana, kusaidiana. Kuwa na maamuzi Bora Kwa wakati sahihi.
Na hayo yote watajifunza kupitia vile unavyoishi na Mwenza wako(Mkeo au mumeo). Mtoto hafundishwi Kwa maneno isipokuwa Matendo yenu.
Ukiminya haki za mwenza wako basi hata watoto wako wataminya Haki zako. Hiyo ni Hakika na kweli. Hayo nimeyaona Kwa macho yangu wala sijahadithiwa.
Ufanyaji kazi na uwekezaji ni hatua ya pili ya namna ya kukabiliana na nyakati hatari za Wakati ujao. Hatuwezi kujiongopea kuwa Hatutazeeka ilhali tunawaona Wazee, na wala hatuwezi kujifariji kuwa tutakufa kabla ya kuwa Wazee huko ni kujipumbaza,
Uwekezaji ni muhimu.
Ununuzi wa Maeneo yenye Rutuba Kwa nyakati zijazo ni muhimu,
Uwekaji wa Akiba ya pesa pia uzingatiwe.
Upandaji wa mashamba ya miti, au ununuzi wa Vito Kama dhahabu iwe sehemu ya akiba.
Katika ngazi ya kitaifa,
i. Ni muhimu kubadilisha mifumo yetu ya uendeshaji nchi, viongozi wasio na msaada wafukuzwe,.
ii. Ubadilishaji wa Katiba inayoendana na mawazo ya kizazi kipya katika ulimwengu ujao ni muhimu, Katiba iliyopo iondolewe.
iii. Sheria kandamizi zinazobana Wanaume ziondolewe,
Na zile zinazokandamiza Wanawake ziondolewe. Pia sheria ziseme wazi kuwa hakuna USAWA baina ya Mwanamke na Mwanaume.
iv. mpango wa lazima wa Kuvamia Mataifa mengine na kujipatia Mali Kwa ajili ya taifa letu uundwe na utekelezaji wake usimamiwe na viongozi wenye akili na maono ya miaka Mia mpaka Mia tatu mbele.
Lazima tupate kiongozi mwenye falsafa na mtazamo Kama huo ndipo taifa letu litaweza kuendelea.
v. Mpango wa Siri wa kuhakikisha Uchumi unashikiliwa na Wazawa ndani ya nchi uzingatiwe. Kuondoa viongozi vibaraka wa wageni. Tusipowahujumu basi tutahujumiwa. Ndio dunia iko hivyo.
Vi. Kuondoa mawazo ya uchamachama sijui UCCM na UCHADEMA, Ila uwepo utaifa mbele.
Moja ya Dalili ya kuwa taifa bado watu wake hawajitambui na Masikini ni kuendekeza uchama badala ya utaifa. Hii inatokana na ubinafsi na uroho Kama sio ulafi wa Mali za nchi.
Nipumzike sasa.
Sabato NJEMA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam