Wazee wetu nguli wa Siasa Mzee Kinana na Mzee Makamba kurudi kwenye chati na kuendelea kuheshimika?

Wazee wetu nguli wa Siasa Mzee Kinana na Mzee Makamba kurudi kwenye chati na kuendelea kuheshimika?

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,635
Reaction score
2,271
Wadau mtakumbuka jinsi wazee wetu hawa walivyodhalilishwa na watu walio wachanga sana kisiasa hapa nchini, dharau hizo zilizidi hasa katika Serikali ya awamu ya tano.

Je, sasa si wakati wa wazee wetu hawa kurudia kuheshimika kutokana na hazina yao ya kisiasa hapa Tanzania? Karibuni kuchangia mada hii.
 
Issue sio Kurudi kwenye Chati, na Heshima Yao Iko Pale Pale " Mbabe wao si unajua is no more", So wazee awa Wasadie Kuboresha Siasa za Maridhiano zilizoaribiwa na huyo "Mbabe'. Wasaidie Ndani ya Chama Chao, Tujenge Taifa lenye watu wenye Kuheshimiana, Kupendana na Kuvumiliana. Ubabe Hauna Tija na Unakuwaga na Mwisho Mbaya.
 
Hao wazee hawana maana yeyote waache wapumzike kama kuiba hela za uma washaiba sana unataka nini zaidi? Badala ya kuwafikiria wazee vijijini huko.
 
Uzee nao inabidi ukija uheshimiwe, huwezi shindana nao, wakati mwingine akili inataka lakini mwili hautaki.
 
Issue sio Kurudi kwenye Chati, na Heshima Yao Iko Pale Pale " Mbabe wao si unajua is no more", So wazee awa Wasadie Kuboresha Siasa za Maridhiano zilizoaribiwa na huyo "Mbabe'. Wasaidie Ndani ya Chama Chao, Tujenge Taifa lenye watu wenye Kuheshimiana, Kupendana na Kuvumiliana. Ubabe Hauna Tija na Unakuwaga na Mwisho Mbaya.
Hizi akili CCM hazipo, MaCCM ni watu walafi sana. watarudi kwa matumbo yao, sio kujenga nchi. CCM ni LAANAKUM.
 
Wote ni bure kabisa; angalau hata msekwa au Warioba na Msuya. Hawa walikuwa ni wachumia tumbo tu, mzee Makamba aliwahi kutuambia kuwa yeye alizaa watoto watakaokuwa mawaziri, yaani alituona sisi watanzania milioni 60 hatuji kuzaa viongozi isipokuwe yeye.
 
Bashiru na Mangula mko wapi mumkalishe kanali na Luteni wa jeshi kwenye kiti Moto?
 
Wadau mtakumbuka jinsi wazee wetu hawa walivyodhalilishwa na watu walio wachanga sana kisiasa hapa nchini, dharau hizo zilizidi hasa katika Serikali ya awamu ya tano.

Je, sasa si wakati wa wazee wetu hawa kurudia kuheshimika kutokana na hazina yao ya kisiasa hapa Tanzania? Karibuni kuchangia mada hii.
Hazina ipi? Wazee wapi hao wanaoteta viongozi wakubwa wa nchi..wazee gani waliokuwa wanaiba nyara za serikali na kufanya biashara ya meno za tembo..tembo walipukutika wengi sana kipind hao unaowaita wazee wameshika nchi..jpm alivyoingia tembo zikaongezeka kama mbuzi na swala..acheni upuuz kushabikia majina ya watu bila kuona uhuni waliokuwa wanaufanya..
Kwanza wengine sio raia wa tz..wamejipenyezaa tu kutoka huko usomalini..
 
Kwahiyo malengo ya Taifa hili ni baadhi ya watu kuheshimika??

Duuh, basi sawa.

Ingawa sio sawa.
 
Back
Top Bottom