Waziri abaini wizi kwenye korosho

Waziri abaini wizi kwenye korosho

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza, amebaini wizi katika zao la korosho mkoani Pwani unaofanywa na watendaji wa vyama vya ushirika na ngazi nyingine, ikiwamo wizara yake.

Chiza alibaini wizi huo juzi wakati wa mkutano wake na wakulima na wadau wengine wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha na kueleza kuwa hali hiyo imesababisha zao hilo kudidimia.


Kutokana na suala hilo, alisema serikali haitamwonea aibu mtendaji yeyote atakayebainika kufanya wizi katika zao hilo kwa namna moja au nyingine zaidi ya kumchukulia hatua za kisheria.


Alitolea mfano wa ubadhirifu huo akisema baadhi ya watendaji wamekuwa wakifanya hujuma kwenye mizani katika upimaji wa korosho kwani zinapopelekwa huonesha kuwa na uzito mkubwa lakini zinapotoka uzito hupungua, hali ambayo inasababisha wasiwasi kwa wakulima.


“Utendaji wa kwenye maghala unachangia wizi, niliwahi kuulizwa Mtwara, huyu mtu anayeitwa stakabadhi ghalani ni nani? Mi nadhani njia nyingine ya kulitazama hili ni kulikagua, kuna haja kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa

Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mfumo mzima ili tujue nani aliyejificha katika kichaka hiki,” alisema.

Chiza aliongeza kuwa kuna vyama kama vile KORECU ambavyo utendaji wake ni mbovu na haiingii akilini kwamba korosho chafu na mbaya zitoke Pwani pekee pia kuwa na takwimu zisizo sahihi kuhusu zao hilo kitaifa, hivyo suala hilo lazima liangaliwe.

Katika hilo alisema takwimu za korosho zilizouzwa India zinaonesha idadi kubwa ya zao hilo kuliko zilizopo hapa nchini hivyo lazima kuna wizi unaofanyika.


Awali Mrajis wa Mkoa wa Pwani, Hadija Mang’era, alisema inakadiriwa kuwa mkoa huo una miti ya mikorosho milioni 10 na kati ya hiyo asilimia 30 sawa na mikorosho milioni tatu ndiyo inayopata huduma za wastani na kuzalisha wastani wa kilo tano kwa mti wakati asilimia 70 iliyobaki iko porini na haitunzwi.



Alisema endapo mikorosho yote milioni 10 ingehudumiwa na kuzalishwa angalau wastani wa kilo 10 kwa mti, ungeuwezesha mkoa huo kuzalisha tani 30,000 kwa mwaka ambazo zingeingiza sh bilioni 21 ikilinganishwa na wastani wa uzalishaji sasa wa tani 12,000 ambazo huwapatia wananchi sh bilioni 8.4 kwa bei ya wastani ya sh 800 kwa kilo.
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=46997


 
Back
Top Bottom