Pre GE2025 Waziri Abdallah Ulega na DC Khadija Nasir Wakabidhi Madawati 3,000 kwa Shule za Msingi na Sekondari Mkuranga

Pre GE2025 Waziri Abdallah Ulega na DC Khadija Nasir Wakabidhi Madawati 3,000 kwa Shule za Msingi na Sekondari Mkuranga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Naona bwana mkubwa Ulega anaendelea kujitengenezea mazingira ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025. Yani yupo tayari kusomesha wanafunzi.

Haya tunasubiri tuone itakuwa mwendelezo au ndiyo lambisha utamu wa asali tu kwa muda. Muda utaongea vizuri!
===================

Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega na Mkuu wa wilaya hiyo, Khadija Nasir wamekabidhi madwati 3,000 kwa shule za msingi na sekondari ikiwa ni mkakati wa kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu.

Madawati hayo yametolewa leo Ijumaa, Januari 10,2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkuranga, ikiwa ni siku chache kabla ya shule kufunguliwa rasmi Januari 13, 2025.

Soma Pia: Waziri Ulega: Tunafanya kazi usiku na mchana kulinda amani

Katika hafla hiyo Waziri Ulega ameahidi kutoa kiasi cha Sh50 milioni kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu na yatima.

Snapinsta.app_473318690_4045832615688963_959657008250277522_n_1080.jpg
Screenshot 2025-01-10 151927.png
 
Back
Top Bottom