Waziri anapotumbuliwa anapaswa kumshukuru Rais kupitia mitandao ya kijamii kama wanavyofanya wanapoteuliwa, kukaa kimya ni kiburi

Waziri anapotumbuliwa anapaswa kumshukuru Rais kupitia mitandao ya kijamii kama wanavyofanya wanapoteuliwa, kukaa kimya ni kiburi

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Tanzania na Afrika kwa ujumla hatuna tabia yakukiri kushindwa au kukosa uungwaji mkono. Tumejaaliwa kiburi kinachoambatana na kujipendekeza.

Mawaziri kama Januari Malamba na Nape Nauye wameaminiwa sana kwenye wizara mbalimbali. Wakati wakiwa kwenye uwaziri walimwita Mhe. Rais Mama na siyo Rais.

Katika tamaduni za Afrika na Dunia ni vigumu kumfanyia kiburi na kumkosoa mama yako adharani. Nilitegemea Mama SSH angeendelea kuwa mama kabla ya uteuzi wao, baada ya uteuzi wao na pale alipowatengua.

Nilitegemea wawe wa kwanza baada ya taarifa kutoka tu waandike kwa umma kumshukuru mama kwa kuwaamini miongoni mwa watanzania wengi. Nilitegemea wamtie mama moyo kwamba pale waliposhindwa kutimiza wajibu watajirekebisha wawe bora zaidi.

Nasikitika kuona vijana hawa wakiondoka ofisini na kwenye mitandao ya kijamii kama vile wameonewa. Nashangaa vijana hawa kujiona wao ni watoto bora kuliko watoto wengine wa mama.

Ndugu zangu, tujifunze kujishusha. Mama angependa zaidi kuwaona mkishirikiana naye adharani kuliko kushirikiana naye gizani. Mama angependa kuona mnabaki na roho nyeupe kabla na baada ya ajira.

Kufutwa kazi siyo kigezo cha kushindwa kufanya kazi. Mfumo wa utumishi wa umma upo sawa na mchezo wa mpira wa miguu; upo wakati mchezaji tegemeo anakaa benchi kuruhusu mchezaji mwingine aingie kwa kuzingatia na mahitaji ya wakati.

Nimezungumza na Nape lakini pia ujumbe huu uwafikie wengine wote wanaoona kutumbuliwa ni kudharauliana au kushushwa kiwango. Ukimya wa vijana hawa upo sawa na kelele za Peter Msigwa.

Tofauti ya Peter Msigwa na akina Nape ni kwamba Mbowe siyo Rais kwa hiyo hakuna dola nyuma yake na hata akimtukana dola itamlinda. Ila akina Nape na Januari wanatumbuliwa na mwenye dola hivyo kuwawia vigumu kutukana adharani badala yake wanatokana gizani kama walivyomtukana JPM.

Tujifunze kwa Joe Biden; kuna majira na nyakati zisizokufaa wewe
 
Yule roboti wake ameondoka nae au bado amebaki wizarani?
20240722_072750.jpg
 
Tanzania na Afrika kwa ujumla hatuna tabia yakukiri kushindwa au kukosa uungwaji mkono. Tumejaaliwa kiburi kinachoambatana na kujipendekeza...
Watumbuliwa pia wanaweza kujiunga CUF ili kupambana CCM.
BAdo wana nafasi kuliko kukaa kwenye comfort zone.

NAPPE ameshahama mikocheni amwachie waziri mwengine?
 
Wachawi mko wapi tuĵane...kutumbuliwa Nape kumekupeni furaha,fine, sasa km mtu mmoja ameleta furaha namna hii je CCM ikitumbuliwa yote?
 
Tanzania na Afrika kwa ujumla hatuna tabia yakukiri kushindwa au kukosa uungwaji mkono. Tumejaaliwa kiburi kinachoambatana na kujipendekeza...
Binafsi huwa najiuliza, ikitokea umetumbuliwa kabla ya mshahara haujatoka, huwa wanlipwa kabisa au ndiyo basi tena...?
 
Back
Top Bottom