Waziri Anthony Mavunde Amesema Makusanyo Sekta ya Madini Imevunja Rekodi

Waziri Anthony Mavunde Amesema Makusanyo Sekta ya Madini Imevunja Rekodi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AMESEMA MAKUSANYO SEKTA YA MADINI IMEVUNJA REKODI

Mavunde apiga marufuku wageni kuingia leseni za wachimbaji wadogo

Atangaza kiama kwa watumishi wasio waadilifu

Kuendesha operesheni maalum, RMO’s mguu sawa

WAZIRI wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameweka wazi makusanyo ya maduhuli kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambayo ni Shilingi Bilioni 753 huku akipiga marufuku kwa wageni kuingia kwenye leseni za wachimbaji wadogo.

Mavunde pia ametangaza operesheni maalum kwa watumishi wasio waadilifu na kumtaka Katibu Mkuu wa Wazira ya Madini Mhandisi Yahya Samamba kuwachukulia hatua za haraka atakapowasilisha majina ya watumishi hao.

Akizungumza Julai 28, 2024 mjini Dodoma, Mhe. Mavunde amesema katika kipindi cha Mwaka 2023/2024, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ilipanga kukusanya jumla ya Sh Bilioni 882.121 kutokana na vyanzo vilivyoainishwa katika Sheria ya Madini Sura ya 123.

Amevitaja vyanzo hivyo ni pamoja na Mrabaha, Ada ya Mwaka ya Leseni, Ada ya Ukaguzi wa Madini, Ada za Kijiolojia, Tozo ya Huduma ya Maabara na malipo ya adhabu mbalimbali.
-
Amesema, katika kipindi cha kuanzia Mwezi Julai, 2023 hadi Juni 30 2024, Tume ya Madini ilikusanya jumla ya Shilingi Bilioni 753.815 sawa na asilimia 85.45 ya lengo la makusanyo lililopangwa.

“Makusanyo haya ni sawa na ongezeko la kiasi cha Shilingi Bilioni 76.080 ukilinganisha na fedha zilizokusanywa katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 ambapo makusanyo yalikuwa ni Shilingi Bilioni 677.734 kwa lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 822.018,” amesema Mhe. Mavunde

Mhe. Mavunde amesema kuanzia Mwaka wa Fedha 2019/2020 hadi 2023/2024, makusanyo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na kutupa imani ya kufikia malengo ya kukusanya Shilingi Bilioni 999.998 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

“Hapo nyuma kidogo, Wizara ilikuwa ikikusanya kiasi kidogo cha maduhuli ukilinganisha na sasa, mathalan, Mwaka wa Fedha 2014/2015, Wizara ilikuwa na lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 209.957 na kufanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 168.043.”Amesema Mh Mavunde.

Aidha, amesema Mwaka wa Fedha 2015/2016 lengo la makusanyo lilikuwa ni Shilingi Bilioni 211.957 na kufanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 207.917.

"Ni marufuku wageni wenye leseni kubwa za biashara ya madini (dealer’s Licence) hususan wa madini ya vito kwenda machimboni kutafuta madini. Kazi hii inafanywa na watanzania pekee wenye kumiliki leseni za broker," Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.

"Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini, Sura 123 kimeweka wazi kwamba, kwa mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji wa madini, pale atakapohitaji msaada wa kiufundi ambao haupatikani nchini, anaruhusiwa kuingia makubaliano na mgeni kutoka nje ya nchi kupata huduma hiyo baada ya makubaliano hayo kupitishwa na Tume ya Madini," Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-08-02 at 15-34-31 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-34-31 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    798.3 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-35-01 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-35-01 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    539.2 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-07 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-07 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    745.8 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-15 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-15 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    691.2 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-22 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-22 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    700.7 KB · Views: 7
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-28 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-28 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    690.3 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-32 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-32 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    749.3 KB · Views: 7
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-37 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-37 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    666.2 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-08-02 at 15-37-41 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    Screenshot 2024-08-02 at 15-37-41 Wizara ya Madini (@wizara_ya_madini_tanzania) • Instagram ph...png
    738.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom