John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wizara ya Maji imeitaka kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza mabomba kwenye ujenzi wa miradi ya maji Kanda ya Ziwa inayotekelezwa na Serikali kupitia fedha za Uviko 19, kuhakikisha inafikisha mabomba hayo kwa wakati kwenye maeneo ya miradi.
Lengo ni kuepuka kukwamisha miradi hiyo na hatimaye lengo la Serikali la kuwafikishia wananchi maji safi na salama liweze kufikiwa.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa rai hiyo wakati akikagua mradi wa maji wa Bunamala Mbugani wilayani Itilima mkoani Simiyu na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.
“Upande huu wa Kanda ya Ziwa nitoe wito, Kampuni ya Kahama Oil Mills Ltd tafadhali msitukwamishe kusambaza mabomba kwa wakati, tunahitaji mabomba kwa wakati kama mlivyosaini mkataba.
“Wanashindwa kumalizia lile tank lakini wanashindwa kwa sababu mabomba hayajafika, kwa kuwa tupo ndani ya muda ninasisitiza kila kitu kije kwa wakati,” alisema Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Amesema katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19, ni lazima wananchi wahakikishiwe upatikanaji wa maji safi na salama ambayo yatawasaidia kujikinga na maradhi hayo.