Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Zikiwa zimepita saa chache tangu Mwananchi iripoti wanawake katika Kijiji cha Oltepes kilichopo Kata ya Orbomba, wilayani Longido kutumia mkojo wa ng’ombe kujisafisha wakiwa hedhini kutokana na ukosefu wa maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema analifanyia kazi.
Akijibu changamoto hiyo katika ukurasa wa Instagram wa Mwananchi (@mwananchi_official) leo Jumanne Novemba 12, 2024, Aweso ameandika: “Nakiri kulipokea jambo hili na niahidi baada ya kulifuatilia kwa undani wake Wizara ya Maji utalitolea ufafanuzi yakinifu.”
Soma Pia: Ukosefu wa maji: Watumia mkojo wa ng'ombe kujisafisha wakiwa hedhini
Eneo hilo lenye wakazi wapatao 4,000, hutembea umbali wa kilomita tano kutafuta maji, lakini nyakati za kiangazi wanapolazimika kutumia mkojo wa ng’ombe, hutembea mpaka kilomita 10 kutafuta maji ya kunywa na kupikia kwenye mabwawa.