Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, ametoa siku saba kwa wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Maji wa Miji 28 wilayani Muheza mkoani Tanga, kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo kutokana na kuonekana kusuasua licha ya uwepo wa fedha za mradi huo.
Waziri Aweso amebainisha haya baada ya kufika katika Kata ya Kilulu wilayani humo, kukagua mradi huo na kuelezwa changamoto ya maji na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Zainab Abdallah, pamoja na wananchi wengine wa Muheza, ambapo Waziri Aweso amesema hajaridhishwa na kasi ya mradi huo Muheza licha ya mradi kama huo kutekelezwa vyema katika maeneo mengine kama Korogwe na Handeni.
Soma Pia: Tanga: Waziri Aweso Akagua Mradi wa Maji wa Bilioni 170 Katika Kata ya Mswaha