Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Nakuja kwenu Afisa Maji wa kujiteua mwenyewe kwa wakazi wa Mbezi Beach na Dar kwa ujumla.
Kiukweli Dar kuna upungufu mkubwa wa maji, yaani kadri siku zinazovyoenda hali inazidi kuwa mbaya. Kama sisi wa Mbezi Beach sasa hivi ni kupata maji kwa masaa mamache yanasepa, ukitoa taarifa majibu ni yale yale, tuna shughulikiwa, tumepokea changamoto hiyo, kulikuwa na presha ndogo tutashughulikia, nk.
Yaani unaripoti mnakaa siku tatu nne maji yanarejea, baada ya masaa machache yamesepa, au yatarejea na kudumu kwa siku mbili tatu yakiwa na presha ndogo sana halafu yanakata mazima!
Nadhani tunaona vilio vya kutosha kwa wakazi wa Ubungo, Tabata, Kimara, Malamba Mawili na maeneo mengine, inashangaza Waziri Aweso Wizara ya Maji anakuja kusema huduma ipo ya uhakika na maji yapo lakini mtaani hali ni tofauti, hatuyaoni maji hayo.
Je, Waziri anapotoshwa kwa kupewa taarifa za uongo? Au anajua kuna upungufu wa maji lakini anashindwa jinsi ya kulileta kwa wananchi, maana mvua zilipiga za kutosha na maji yalivunywa mpaka mengine yakaachiliwa yasije kubomoa ukuta
sasa huu upungufu tunaopitia unatoka wapi?
Waziri Aweso Wizara ya Maji tunakwambia kila leo achana na kwenda ofisi za DAWASA wakudanganye, pitia comments kwenye mitandao ya kijamii kila maji au wizara yako inapotajwa, lakini pia pita mtaani kwenye maeneo yanokolalamikiwa kila leo na usikie wananchi wana nini cha kusema, hapo utapata uhalisia wa nini wananchi wanapitia juu ya huduma hii. Halafu urudi huko ofisini kuangalia shida iko wapi, kama ni hujuma inatokea wapi, na kama ni upungufu toa taarifa watanzania wajue, na utuambie una mpango gani kuhakikisha wananchi hawaathiriki na hili.
Acha kuchukua majibu ya kukopi na kupesti, ukweli huduma za DAWASA sasa hivi ni takataka, na wewe kama Waziri una kazi kubwa mbele yako kuhakikisha huduma hii inakuwa ya uhakika Wizara ya Maji na siyo kutupa majibu ya kisiasa!
Pia soma
- KERO - Vilio shida maji: Wananchi Dar wadai kuona kwenye Tv Rais kumtua mama ndoo ila hawajui inatuliwa wapi
Nakuja kwenu Afisa Maji wa kujiteua mwenyewe kwa wakazi wa Mbezi Beach na Dar kwa ujumla.
Kiukweli Dar kuna upungufu mkubwa wa maji, yaani kadri siku zinazovyoenda hali inazidi kuwa mbaya. Kama sisi wa Mbezi Beach sasa hivi ni kupata maji kwa masaa mamache yanasepa, ukitoa taarifa majibu ni yale yale, tuna shughulikiwa, tumepokea changamoto hiyo, kulikuwa na presha ndogo tutashughulikia, nk.
Yaani unaripoti mnakaa siku tatu nne maji yanarejea, baada ya masaa machache yamesepa, au yatarejea na kudumu kwa siku mbili tatu yakiwa na presha ndogo sana halafu yanakata mazima!
Nadhani tunaona vilio vya kutosha kwa wakazi wa Ubungo, Tabata, Kimara, Malamba Mawili na maeneo mengine, inashangaza Waziri Aweso Wizara ya Maji anakuja kusema huduma ipo ya uhakika na maji yapo lakini mtaani hali ni tofauti, hatuyaoni maji hayo.
Je, Waziri anapotoshwa kwa kupewa taarifa za uongo? Au anajua kuna upungufu wa maji lakini anashindwa jinsi ya kulileta kwa wananchi, maana mvua zilipiga za kutosha na maji yalivunywa mpaka mengine yakaachiliwa yasije kubomoa ukuta

sasa huu upungufu tunaopitia unatoka wapi?Waziri Aweso Wizara ya Maji tunakwambia kila leo achana na kwenda ofisi za DAWASA wakudanganye, pitia comments kwenye mitandao ya kijamii kila maji au wizara yako inapotajwa, lakini pia pita mtaani kwenye maeneo yanokolalamikiwa kila leo na usikie wananchi wana nini cha kusema, hapo utapata uhalisia wa nini wananchi wanapitia juu ya huduma hii. Halafu urudi huko ofisini kuangalia shida iko wapi, kama ni hujuma inatokea wapi, na kama ni upungufu toa taarifa watanzania wajue, na utuambie una mpango gani kuhakikisha wananchi hawaathiriki na hili.