Waziri Aweso: Rais, anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo yake

Waziri Aweso: Rais, anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo yake

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani mkoani Tanga, Jumaa Aweso amesema kukamilika kwa Daraja la Mto Pangani na Barabara ya Tanga- Pangani- Saadani- Bagamoyo kutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wilaya hiyo na Mkoa wa Tanga kwa ujumla na hivyo kukuza uchumi wa mtu binafsi na wa mkoa.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilayani Pangani Februari 26, 2025, Waziri Aweso amesema kukamilika kwa mradi huo pia kutasisimua utalii wa Mbuga ya Saadani yenye sifa ya kuwa hifadhi pekee ya wanyama iliyo pembezoni mwa bahari barani Afrika.

Waziri Aweso pia amemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni humo, akikumbusha kuwa ni Rais Dkt. Samia aliyeidhinisha na kutoa bilioni 2.4 za kujenga kingo kwenye Bahari ya Hindi upande wa Tanga ili kuondoa adha ya maji kufurika na kuharibu makazi na mashamba ya wakazi wa mkoa huo.

 
Back
Top Bottom