BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Naomba Serikali kupitia Waziri wa Maji, Juma Aweso afuatilia chanzo cha Wakazi wengi wa Mkoani Morogoro kukosa huduma ya maji.
Hii hali inatutesa sisi wakazi wa Morogoro kwa muda mrefu sasa, tumekuwa tukipiga kelele kwa mamlaka lakini ni kama hatusikilizwi.
Baadhi ya Watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) hawatimizi majukumu yao na hawatoi taarifa stahiki, kwa ufupi ni kuwa kuna mgao wa maji ambao ni mkali na hatuambiwi nini kilichotokea au kinachoendelea kutokea.
Taarifa zilizopo mitaani ambazo sio rasmi japo unaweza kuzifikiria kwa jicho la tatu kuwa zina ukweli ni kuwa inadaiwa Waziri Aweso ana ukaribu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji ya Moro kiasi kwamba anakuwa mzito pia katika kumuwajibisha au pengine Aweso hapewi taarifa sahihi.
Namuomba Aweso hicho anachokifanya kuzunguka kwenye mamlaka mbalimbali wa DAWASA ambapo amenukuliwa akisema kuwa kuna hujuma na uzembe kwenye uwajibikaji, basi aje huku Morogoro ndio atajua hajui.
Baadhi ya maeneo ambayo huduma ya maji ni kero ni; Kata za Kihonda, Kichangani, Tungi, Mkundi, Mindu na Kilakala.
Pia soma ~ Waziri Aweso ateua Mkurugenzi Mpya wa Maji Morogoro, aelekeza iundwe timu maalum ya Wataalam
TBC1 nao wameripoti juu ya changamoto ya maji iliyopo Morogoro
Ufafanuzi wa MORUWASA ~
MORUWASA: Tuna upungufu wa uzalishaji maji kwa 49% ndio maana Morogoro kuna mgao
MREJESHO:
Waziri Aweso: Bwawa la Mindu ni roho ya Wananchi wa Morogoro. Watu kukosa maji wiki 3 Morogoro ni uzembe. MORUWASA Msikae Ofisini
NA
- Meneja wa usambazaji maji MORUWASA asimamishwa kazi

===============================