Waziri Bashe atua kibabe Kisesa na kukutana na Mbunge Luhaga Mpina ana kwa ana

Waziri Bashe atua kibabe Kisesa na kukutana na Mbunge Luhaga Mpina ana kwa ana

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (mb) atua kibabe Kisesa na kukutana na Mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina ana kwa ana.

Amtaka mbunge huyo kuacha siasa katika zao la Pamba Kwani Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, inahitaji kuona fedha zinazotengwa zinanufaisha wakulima.

Awaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa serikali inarejesha kitalu cha mbegu kuwapatia ruzuku ya dawa za wadudu katika zao la mahindi na pembejeo na mbegu katika zao la Pamba.

Wazee wa kimila wamsimika kuwa Mtemi (Chief) wa jimbo hilo.

Kihongosi aunguruma asema hataki siasa chafu mkoani humo kwani ametumwa kazi ya maendeleo na Rais Samia hivyo hayupo tayari kuona siasa katika kilimo.

Mpina asema yuko tayari kuweka tofauti zake na Bashe pembeni na kuungana katika masuala ya maendeleo na shughuli za serikali.

Bashe ametua jimboni humo katika mkutano na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kufunga mashindano ya michezo mbalimbali ya Mwandoya na kupokelewa na mamia ya wananchi.

Ametumia fursa hiyo kukutana na Mbunge Mpina ambapo amemtaka kuacha siasa katika zao la Pamba kwa maslahi ya wananchi.

Soma Pia:
“Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kilimo Mpina amesema hapa na mimi nataka nisisitize tuweke mambo mengine pembeni aache siasa na sitaki siasa katika zao la Pamba, nafahamu zipo changamoto lakini tulipotoka sio tulipo sitakubali mtu arudishe nyuma jitihada hizi wanaoteseka wananchi,”alisema.

Aidha amekabidhi trekta 40 kwa jimbo hilo na kuwataka maafisa kilimo na ugani kuacha kukaa mjini na kuishi vijijini ili waweze kuwasaidia wakulima utaalamu na kufikia malengo ya serikali ya kilimo chenye tija.

Amewashukuru wazee wa kimila kwa kumsimika kuwa mtemi wa jimbo hilo.

“Nami leo nimesimikwa kuwa mtemi wa Kisesa hivyo Mpina akinitambia pale bungeni kwa kuingia na fimbo ya uchifu nami nitaingia na yangu,”amesema.

Naye Mkuu wa mkoa huo Kennan Kihongosi amemuhakikishia Waziri Bashe kuwa yeye ndio mwenye dhamana na mkoa huo, hivyo hawezi vumilia watu wanaotafuta umaarufu katika siasa kuingiza masuala ya maendeleo.

“Nimetumwa kazi na Rais Dk. Samia, Simiyu ni ya kwanza ama ya pili katika kuzalisha pamba hivyo kwa wananchi ni zao la kiuchumi sitaki wanasiasa watumie zao hilo kutafuta umaarufu shida zinazosemwa katika zao hilo si za kweli wananchi wa Kisesa msikubali kutumika,”amesema

Naye Mbunge Mpina ametumia fursa hiyo kumkaribisha Bashe Kisesa na kueleza kuwa wanazo tofauti zao hali iliyowafikisha hadi Mahakamani lakini yupo tayari kushirikiana naye katika masuala ya utendaji wa serikali.

IMG_20240913_201204_928.jpg
IMG_20240913_201201_507.jpg
IMG_20240913_201158_883.jpg
IMG_20240913_201155_406.jpg

IMG_20240913_201851_857.jpg
 
Bashe umechemsha ,yaani umepitisha bajeti halafu unataka kuificha?Yaani katiba yenu munaikanyaga Kwa nguvu zenu,huu ulikuwa ubaguzi ambao bashe ilibidi ujiuzulu ,Yale Yale ya mwigulu kutaja watu wahamie Burundi nyie mawaziri ni vichaa ,yaani Raia walipe Kodi halafu wewe ulete usomali wako pumbafuuu bashe!!
 
Hizo trekta ni za serikali au watu binafsi, mtu alime heka moja kwa 35k...labda kama anaweka mikojo kwenye hilo trekta
 
Tatizo la CCM watu wengi ni wanafiki ni chama ambacho wale wote wanajifanya wanakipenda wala hawakipendi wao wanafaidika na CCM Kuwa madarakani maana wanaiba kwa mgongo huo na ndio mana hata polisi wanaweza kufanya mambo ya kishenzi kwa Watanzania wenzao ili wafurahishe baadhi ya watu kwa kutojitambua.

Askari wote nchi hii wanaishi maisha duni sana lakini angalia wanayotenda kwa raia wenzao,Mtu kama Mafwele anatuhumiwa kufanya ukatiri mwingi lakini hajakamatwa kwasababu wote CCM na polisi wanategemeana ila tungekua na sheria nzuri zikatenganisha huu mnyororo tungekua mbali kama nchi.

Unafiki ni mkubwa sana nchi hii wale Wabunge wanamwakilisha nani? ikiwa wamekaa tunalipa kodi wanalipwa wakiambiwa mtu anatekwa anauawa kibibi kile kinagoma halafu kinatwiti mtu akiuwawa wote ni ujinga. Ndio mana unaweza kusikia Waziri anasema Sehemu flani ya Nchi haitapata huduma kwasababu ya maamuzi yake tu wakati hiyo sehemu inalipa kodi kabisa na hafukuzwi kazi...
 
Waziri wa Kilimo Mh Bashe na Mbunge wa Kisesa Mh Mpina wamesema wanaweka Siasa pembeni Ili waweze kuwaletea maendeleo Wananchi
---
Baada ya kutoleana vijembe ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatimaye Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina wamekutana uso kwa uso.

Bashe yupo kwenye ziara ya kikazi kwenye maeneo mbalimbali nchini na leo Ijumaa, Septemba 13, 2024 amefika katika Jimbo la Kisesa linaloongozwa na Mpina na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wakulima na maofisa ugani.

Akiwa jimboni humo, Bashe amemtaka Mpina kuacha siasa kwenye zao la pamba kwa kuwa Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, inahitaji kuona fedha zinazotengwa zinanufaisha wakulima wa zao hilo.

“Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kilimo, Mpina amesema hapa na mimi nataka nisisitize tuweke mambo mengine pembeni, aache siasa na sitaki siasa katika zao la pamba.

Nafahamu zipo changamoto lakini tulipotoka sio tulipo, sitakubali mtu arudishe nyuma jitihada hizi wanaoteseka wananchi,” amesema Bashe na kuongeza: “Na mimi leo nimesimikwa kuwa mtemi wa Kisesa, hivyo Mpina akinitambia pale bungeni kwa kuingia na fimbo ya uchifu nami nitaingia na yangu.”

Katika ziara yake jimboni humo, Bashe amekabidhi trekta 40 huku akiwataka maofisa kilimo na ugani kuacha kukaa mjini na kuishi vijijini ili kuwasaidia wakulima na kufikia malengo ya Serikali ya kukifanya kilimo chenye tija.

Pia, ameahidi kuwa Serikali itarejesha kitalu cha mbegu kuwapatia ruzuku ya dawa za wadudu katika zao la mahindi na pembejeo za pamba.

Kwa upande wake, Mpina amesema yuko tayari kuweka pembeni tofauti zake na Bashe na kuungana kwenye masuala ya maendeleo.

Amesema anatambua kuwa wana tofauti na Bashe, hali iliyowafikisha hadi mahakamani, lakini yupo tayari kushirikiana naye katika masuala ya maendeleo.

Naye upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kennan Kihongosi amemuhakikishia Bashe kuwa yeye ndio mwenye dhamana na mkoa huo, hivyo hawezi kuvumilia watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuingiza masuala ya maendeleo.

Source: Mwananchi


Mlale Unono 😀
 
Lucas Mwashambwa.
Ulisemaje kuhusu Bashe tena?
 
Back
Top Bottom