Waziri Bashungwa Aanza Ziara ya Kikazi Mkoa wa Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI BASHUNGWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOA DODOMA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo tarehe 19 Januari 2024

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara katika wilaya za Mkoa wa Dodoma na miradi mingine inayotekelezwa katika Sekta ya Ujenzi mkoani humo.

Miradi atakayokagua na kutembelea ni pamoja ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato na Majengo, ujenzi wa Barabara ya Mzunguko (Outer Ring Road), ujenzi wa Barabara ya Ntyuka-Mvumi- Kikombo, barabara ya Hogoro – Machenje - Kongwa, ujenzi wa barabara ya Kongwa - Mpwapwa sehemu ya Mpwapwa - Mwanakianga na Mpwapwa - Ving'awe pamoja na Ukaguzi wa eneo la Mtanana, Kongwa.
 

Attachments

  • GEMn940W4AAi42B.jpg
    292.7 KB · Views: 6
  • GEMn8SmWAAABBTB.jpg
    292.8 KB · Views: 5
  • GEMn94yWQAEL0Fk.jpg
    268.3 KB · Views: 4
  • GEMn_rZXIAAtW0E.jpg
    326.3 KB · Views: 3
  • GEMn_rbWsAAlKT_.jpg
    273.2 KB · Views: 4
  • GEMn_rbXEAA5kA3.jpg
    279 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…