Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Bashungwa ametoa maelekezo hayo Mkoani Lindi wakati akizungumza na Wananchi na kutolea mfano ajali iliyotokea Oktoba03, 2024 nchini Congo ambapo Meli MV Merdi ilizama katika Ziwa Kivu na kusababisha vifo na upotevu wa mali.
“Ni marufuku kwa TEMESA kujaza abiria na mizigo kupita viwango, abiria msikubali kupanda chombo ambacho umeambiwa ujazo umepita ukomo na msiwe wabishi kwani tunafanya hiyo kwasababu tunataka kulinda nguvu kazi ya Taifa letu”, amesisitiza Bashungwa.
Bashungwa ametoa rai kwa wananchi kuwa na subra ya kusubiri kivuko kingine pindi wanapoona Kivuko kimejaa ili kuepusha ajali na matukio kama hayo na kuhakikisha tunalinda na kutunza nguvu kazi ya Taifa
Pia soma
- Waziri Bashungwa: Upotoshaji wa vivuko Kigamboni una maslahi binafsi
- Sehemu ya kusubiria abiria Kivukoni joto ni kali na feni hazifanyi kazi
- Vivuko vimekuwa kero, wanatoa taarifa za ghafla kuwa hamna huduma
- Huduma za Vivuko Kigamboni janga linaloenda kusababisha maafa nchini
- Huduma za Uvushaji wa MV Kigamboni zasitishwa