Waziri Bashungwa, kuhusu Stendi Kuu ya Dar es Salaam, Tusaidie Watanzania

Waziri Bashungwa, kuhusu Stendi Kuu ya Dar es Salaam, Tusaidie Watanzania

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Mhe. Innocent Bashungwa (MB) Waziri wa Nchi OR - TAMISEMI, Hongera kwa kazi nzuri unayofanya ya kuendelea kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Mhe. Waziri abiria waliolalamika au kukataa kushuka pale stendi ya mkoa wa Dar Es Salaam wana hoja ya msingi, tunashukuru kwa kuliona hilo nakuagiza Viongozi wakae na kuliangalia haraka namna ya kutatua.

Mhe. Waziri, kama tatizo ni usalama, na kama magari yanatakiwa kuingia na kukaguliwa ili kujua kama yamebeba Wahamiaji wasio na vibali, tunaomba magari hayo yaingie ili kukaguliwa na kuruhusiwa kuendelea kwenye vituo vyao binafsi kama ambavyo yanapita na kukaguliwa stendi ya Msavu na kuendelea na Safari. Inaumiza kuona umeshuka Stendi ya mkoa wa Dar Es Salaam kisha ukatafuta usafiri wa tax au bajaji baadaye gari ulilopanda toka mkoani linakupita huku likiwa tupu na linaelekea unakoelekea wewe.

Tatizo la msingi ni abiria kuzuiwa kuendelea na gari na wala sio magari kugoma kuingia stendi ya mkoa, Mhe Waziri, ni vyema hizi stendi za watu binafsi zikatumika kama vyanzo vya mapato ya Halmashauri huku mabasi yote yakitakiwa kupita stendi ya mkoa wa Dar Es Salaam.

Mhe. Waziri, ni vyema stendi hizi za makampuni binafsi vikatumika kama chanzo cha Mapato ya ndani ya Halmashauri husika ili kuweza kuongeza wigo wa mapato.

Mhe. Waziri, hongera saana kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa madarasa, Shule, nyumba za walimu, zahanati, vituo vya Afya, Hospital na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, hakika unafanya kazi kubwa saaana, Mwenyezi Mungu aendelee kukupa Afya njema ili uweze kuendelea kuwatumikia Watanzania.

Vijana tutumie fursa iliyopo ya Mikopo isiyo na riba inayoendelea kutolewa na Halmashauri zetu, Serikali kupitia OR - TAMISEMI, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inatoa mikopo kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu zaidi ya Shilingi bilioni 75.98, Fedha hizi zimeshaanza kutolewa katika Halmashauri zote 184.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya usiku na mchana ya kuwatumikia Watanzania.

KAZI IENDELEE.
 
Tatizo hiyo mikopo inatolewa kivikundi
 
Back
Top Bottom