Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bashungwa ameeleza hayo leo Julai 08, 2024 mbele ya wananchi wa eneo la Kazuramimba katika ziara ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ya ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza Mkoani Kigoma.
Aidha. Bashungwa ameeleza kuwa Wizara ya Ujenzi imekamilisha kufanya usanifu wa barabara kuanzia Kibaoni kuelekea Kasulu na hatua iliyopo hivi sasa ni kuendelea kufanya mazungumzo na mfadhili ili nayo iweze kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais nikuahidi Wizara ya Ujenzi hatutakuwa kikwazo kwa dhamira yako ya kusaidia Mkoa wa Kigoma kupata maendeleo, kwahiyo barabara hii ya kibaoni kwenda Kasulu tunaendelea na mazungumzo ili tutakapokamilisha ujenzi wa kilometa 51.1 ya barabara ya Malagarasi - Uvinza basi na kipande cha Kibaoni - Kasulu kianze kujengwa kwa kiwango cha lami”, amefafanua Bashungwa.
ABashungwa ameeleza kuwa Mkoa wa Kigoma utaunganishwa na Mkoa wa Katavi kwa barabara ya lami hivyo wizara ya ujenzi itakamilisha usanifu wa kina wa kilometa 102 zilizobakia ili Serikali iweke katika vipaumbele vyake na kutengewa bajeti.