Waziri Bashungwa na Dkt. Abbas muwe makini na kiki ya Yanga itawatokea puani

Waziri Bashungwa na Dkt. Abbas muwe makini na kiki ya Yanga itawatokea puani

tzkwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
1,568
Reaction score
3,610
Mlitaka kumfurahisha mama kwa kusogeza mechi mbele ili watu waangalie uzinduzi wa kitabu cha Mwinyi pia kumpa mama nafasi ili aje uwanjani. Kiki hii iligonga mwamba.

Kiki ya pili mnataka kuwapa lawama Yanga na TFF wakati UJINGA mmeufanya nyinyi wizarani. Hii kiki ya pili nayo itawatokea puani. Msijaribu kuwapa adhabu Yanga wala TFF, pigeni kimya mmeshalikoroga na watu wote wanajua nyie ndio wachawi wawili (Domo-Chaijaba na Mr.Mishavu).

Kama mna hekima hata robo ombeni msamaha kwa watanzania pia muweke mambo sawa hela zao zinarudi vipi.
 
Hao jamaa ni kichwa maji kweli, wanatanguliza maslahi yao binafsi ya kujipendekeza hawaangalii public interest
 
Kufungia magazeti na radio zinamsifu Mbowe. Siku Mbowe akijiunga CCM anapoteza kibarua chake.
Ndio hapo kuwatofautisha hua nashindwa mmoja anatumbo kama gunia la choroko na mwingine anaongea kama anatema mate chini hua sielewi yupi ni yupi.
 
Pamoja na huu uhuni uliofanywa na viongozi wa serikali lakini aliyefanya kosa kubwa kuliko wote ni Viongozi wa TFF.

TFF walikuwa na uwezo wa kukataa katakata kuairisha au kusogeza mbele muda wa mechi kwa maslahi ya mchezo wa soka.

Kwa kuwa kikao cha mwisho cha mechi (Pre match meeting) kilishafanyika hakukua na namna ya mechi hiyo kusogezwa.

TFF imetuangusha kwa kusikiliza ushauri wa ovyo kutoka kwa watu wasiojua mpira
 
Kibongo bongo huu wote ulikuwa mkakati wa kupiga hela. Mtaongea mwisho wa siku wahusika washachukua mpunga wao.

Mechi haijachezwa hivyo simba waliopaswa kuchukua hela hawatopewa. Hakuna dalili za pesa kurejeshwa kwa kila aliekata ticket hivyo hiyo ni ushindi kwa waliopanga mkakati wote huu. Karibu Tanzania, mwenye kuwahi siku zote ndio mshindi.
 
Acha kuropoka unauhakika gani walitoa orders ili kumfurahisha Mama ?
 
Pamoja na huu uhuni uliofanywa na viongozi wa serikali lakini aliyefanya kosa kubwa kuliko wote ni Viongozi wa TFF.

TFF walikuwa na uwezo wa kukataa katakata kuairisha au kusogeza mbele muda wa mechi kwa maslahi ya mchezo wa soka.

Kwa kuwa kikao cha mwisho cha mechi (Pre match meeting) kilishafanyika hakukua na namna ya mechi hiyo kusogezwa.

TFF imetuangusha kwa kusikiliza ushauri wa ovyo kutoka kwa watu wasiojua mpira
Tanzania kila taasisi ni Tawi la serikali. Hakuna sehemu yeyote ina uwezo wa kupinga maamuzi ya serikali.

Tatizo linakuja kwamba hiyo Serikali ina wasemaji na watoa maamuzi wengi. Kila mwenye madaraka ana kauli. Ndio maana kila siku matamko yanatolewa na kukanushwa.
 
Back
Top Bottom