Waziri Bashungwa na Dkt. Abbas muwe makini na kiki ya Yanga itawatokea puani

Hahaaaa tupeni majina ya hao mnaowataja wanabodi huyo tumbo kubwa na mwenye mashavu kama sijui nini tuwafahamu ikiwezekana mtupie na picha
 
Fifa against Government.
Ushauri wa mleta mada ufatwe,vinginevyo wanakula ban.
 
😂😂😂😂 Mr Mishavu anavaa miwani.
 

Mkuu, kwa dhati ya moyo wako kabisa, unataka kutuaminisha kuwa kuna mtu au taasisi (private or public) yoyote ambayo inaweza kukaidi (privately or publicly) maagizo (maelekezo) ya serikali katika nchi yetu bila kujali yanafaa au hayafai?

Nafikiri ni heri kuunga mkono wito wa PM kuwa tuwe wavumilivu katika wakati huu wakati mamlaka za mpira zikifanya bidii za kutafuta ukweli na kutoa taarifa kwa wananchi.
 
Pamoja na huu uhuni uliofanywa na viongozi wa serikali lakini aliyefanya kosa kubwa kuliko wote ni Viongozi wa TFF.

TFF walikuwa na uwezo wa kukataa katakata kuairisha au kusogeza mbele muda wa mechi kwa maslahi ya mchezo wa soka.
Hatuna details na hatujui ni pressure kubwa kiasi gani viongozi wa TFF walikuwa subjected tu na labda walipambana vipi.

Barua ya TFF ukiicheck between the lines unaweza kuona kitu. Maneno haya “TFF imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda kutoka Wizarani” sio ya kubeza. Huenda hakukuwa na room ya kureason out na wale watu waliocram kumfurahisha boss wao.

Yanga wamefanya sawa kabisa. Lazima tukokeshe huu utaratibu wa watu Serikalini kujiamulia tu kukanyaga kanuni na vifungu vya Katiba
 
Wizara ina mbavu gani za kuziadhibu club?
 
Kweli kabisa.
 
Maelekezo kutoka juu. TFF wapo sahihi.
 
Itabidi CAG aingilie kati
 
Tusubiri tuone. Serikali imeanza 1961 Yanga imeanzishwa 1935.
Mkuu una maana gani!!!!! Serikali imeanza 1961 - Kuongoza Nchi na Yanga imeanzishwa 1935 - kucheza mpira wa miguu. Ebu tupe mantiki ya maono yako.
 
Kwa mantiki hii, viongozi wa TFF wapo ofisini mpaka sasa wanafanya nini?
Kama wanaweza kushinikizwa kuharibu mechi kimakusudi, ni maana ya kuwa viongozi wa chama cha soka?

Suluhisho la kwanza ni kwa viongozi wa TFF kujiuzuru. Haya mambo tukiyachekea sasa, yataendelea kujirudia siku nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…