mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayofanyika katika Uiwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa ili watanzania waweza kusheherekea mafanikio endelevu ya kuingia nchi zenye kipato cha kati wanatakiwa kuwa wa kwanza kutangaza bidhaa zao.
“Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya ya nchi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye kipato cha kati yawe ni matunda kwa watanzania hasa kwa wakina mama na vijana wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania”.
Alisema Mhe.Bashungwa.