Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
ALIYOSEMA WAZIRI WA MADINI MHE. DOTO BITEKO KUHUSU MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA LEO NOVEMBA 5,2021 JIJINI DODOMA
#Mwaka 2009 Serikali ilitunga upya Sera ya Taifa ya Madini na kufuatiwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Baada ya kuonekana kuwepo kwa changamoto kadhaa, Serikali ilifanya mapitio ya Sheria ya Madini 2010 kwa lengo la siyo tu kuimarisha uwezo wa Serikali kuisimamia Sekta ili iweze kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa, bali pia kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa wachimbaji wadogo kwenye shughuli za madini, kuinua sekta ndogo ya uchakataji madini na vilevile kwa lengo la kufungamanisha Sekta ya Madini na Sekta nyingine za uchumi kwa maendeleo ya Taifa.
# Mwaka 2017 yalifanyika marekebisho makubwa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na.7 ya mwaka 2017. Pamoja na malengo mengine ya marekebisho hayo kuliwekwa masharti yatakayowezesha wananchi na Taifa kunufaika zaidi na maliasili ya madini kupitia dhana ya “Permanent Sovereignty over Natural Resources”.
#Mabadiliko hayo pia yalilenga kutambua haki ya ushiriki wa Serikali (Government participation) katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini na umiliki wa hisa kwa asilimia 16 (16% non dilutable free carried interest) katika makampuni ya uchimbaji na Serikali kuwa na Uwezo wa kuongeza ushiriki (Umiliki) mpaka kufikia asilimia 50 kupitia thamani ya vivutio vya uwekezaji na kikodi alivyopewa mwekezaji.
#Serikali imefanya jitihada kubwa za kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali madini, huku tukishuhudia ongezeko la kasi ya ukuaji wa Sekta hii. Kwa mfano, sekta ilikua kwa asilimia 17.7% mwaka 2019 na kuwa ya kwanza kwa ukuaji nchini ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kabla na baada ya Uhuru. historia hii ya Kisera na Kisheria ambayo nimeileza kwa kifupi sana, utaona kuwa mapinduzi makubwa yamefanyika tangu uhuru mpaka sasa ambapo Serikali Kwa upande wa mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019.
#Tofauti na miaka iliyopita kabla ya kufanyika kwa mabadiliko ya Sheria ya Madini mwaka 2017, ushiriki wa watanzania katika uchumi wa madini umeongezeka, mathalan, katika kipindi cha Mwaka 2020/2021 jumla ya kampuni za watoa huduma kwenye migodi 961 sawa na 66% zilikuwa ni za kitanzania na idadi ya kampuni za kigeni zilikuwa 506 sawa na asilimia 34.
#Ikilinganishwa na tulipotoka, hivi sasa Taifa letu lina migodi mikubwa 9; (6 ya dhahabu, 1 wa almasi, 1 wa tanzanite na 1 wa makaa ya mawe). Pia ipo migodi takribani 28 ya uchimbaji wa kati na mingine mingi ya uchimbaji mdogo wa dhahabu, almasi, madini ujenzi, madini ya viwandani na ya vito vya thamani.
#Kwa upande wa Madini adimu ya Tanzanite ambayo yanapatikana nchini kwetu tu, hivi sasa baada ya kuweka udhibiti mzuri wa madini haya ikiwemo ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya Mirerani ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwa kuongeza mapato ya serikali kutoka shilingi millioni 166 kwa mwaka kabla ya kuwepo ukuta hadi kufikia shilingi bilioni 3.9 baada ya ujenzi wa ukuta.
#Yapo mengi ambayo kama Taifa tumefanikiwa kupitia Sekta ya madini ikiwemo; kupandisha uchumi wa Taifa letu, kuongeza ufanisi wa sekta kupitia maboresho ya sheria, kuanzishwa kwa masoko ya madini, kuongeza uwazi na ushiriki wa watanzania katika sekta ya madini.
#Ndani ya kipindi cha miaka 60 ya Uhuru Serikali ilisaini Mikataba ya Ubia na Kampuni ya LZ Nickel ya nchini Uingereza na kuanzisha Kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited yenye Kampuni tanzu mbili ambazo ni Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Tembo Nickel Mining Company Ltd na Kampuni ya Usafishaji wa Madini ya Tembo Nickel Refinery Company Ltd. Mradi huu unatarajia kutengeneza ajira zipatazo 978 na mapato ya Dola za Marekani bilioni 7.54 sawa na shilingi Trilioni 17.35 za kitanzania kwa kipindi chote cha uhai wa mgodi.
# Serikali imetoa ridhaa ya kutolewa kwa Leseni za uanzishwaji wa Mgodi Mpya Mkubwa wa Uchimbaji Dhahabu wa Nyanzanga utakaojengwa kijiji cha Sotta Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza na Mgodi Mkubwa wa uchimbaji madini ya Rare Earth Elements utakaojengwa katika kijiji cha Ngwala Mkoani Songwe. Muda si mrefu mradi mkubwa wa uchimbaji wa Madini ya Graphite utaanza mkoani Lindi huku tayari Kampuni ya Shanta Gold ikiendelea na ujenzi wa Mgodi wa Kati wa uchimbaji Madini ya Dhahabu wa Singida. Haya ni mapinduzi makubwa na mafanikio kwa Serikali katika kipindi hiki cha miaka 60 ikizingatiwa na historia ya mahali tulipotoka.
#Nchi yetu inaendelea kufungua shughuli hizi za uchimbaji na biashara ya madini kwani hadi kufikia Septemba 2021, Leseni hai ambazo zimeshatolewa ni za utafutaji wa madini ni 1,044 ni za utafutaji wa madini, leseni 15 za uchimbaji mkubwa, leseni 161 za uchimbaji wa kati, leseni 34,000 za uchimbaji mdogo na leseni 1561 za biashara ya madini. Kutolewa kwa leseni hizi kunamaanisha kwamba, Serikali inaweza kuongeza mapato zaidi kupitia sekta hii ya madini. Mfano halisi ni Mwaka wa Fedha tulioumaliza mwezi Juni mwaka 2021 ambapo Wizara ilikusanya shilingi Bilioni 584.8 sawa na asilimia 111.03 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 524 ambazo Wizara ilipangiwa na Serikali izikusanye.
#Tangu kuanzishwa kwa masoko ya Madini mwezi Machi, 2019, hivi sasa nchi yetu ina jumla ya masoko ya Madini 42 na Vituo vya Ununuzi wa Madini 59 yaliyoenea katika mikoa mbalimbali. Aidha, kupitia uwepo wa masoko hayo na vituo vya ununuzi, madini yenye thamani ya shilingi trilioni 3.19 yameuzwa na kuiwezesha Serikali kukusanya shilingi bilioni 222.07 kama mrabaha na ada ya ukaguzi tangu kuanzishwa kwake. Ndugu Wanahabari, haya ni Mafanikio makubwa ikilinganishwa na tulipotoka.
#Hivi karibuni kimefunguliwa Kiwanda kikubwa cha kwanza nchini cha Kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery kiwanda ambacho ni cha Ubia kati ya Serikali kupitia Shirika la STAMICO na wabia kutoka Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Singapore. Kiwanda hiki cha kisasa Afrika Mashariki na Kati, kinasafisha dhahabu kwa kiwango cha Kimataifa cha 999 purity na uwezo wa kusafisha kilo 480 kwa siku, kiwanda hiki kinaweza kupanuliwa na kufikia kusafisha hadi kilo 960 kwa siku kulingana na upatikanaji wa dhahabu. Katika mradi huu, STAMICO ina hisa asimilia 25 na wabia wanamiliki asilimia 75 za hisa.
#STAMICO imefanikiwa kutoa Serikalini jumla ya Shilingi bilioni 3.3 zikijumuisha Shilingi bilioni 1.2 za gawio kwa mwaka wa fedha 2020/21 na mchango Serikalini ya jumla ya Shilingi bilioni 2.1 kwa kipindi cha miaka miwili (2) mfululizo.
#Kwa kipindi cha miaka 60 ya uhuru (GST) mpaka sasa imefanikiwa kutambua jiolojia ya nchi nzima kwa asilimia 96. Ikiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji, utunzaji na usambazaji wa taarifa, GST imefanikiwa kuboresha mfumo wa usambazaji wa taarifa/takwimu za jiosayansi. Uanzishwaji wa mifumo hii umerahisisha kwa kiasi kikubwa upatikanaji na usambazaji wa taarifa hizi kwa wadau.
#GST imefanikiwa kufanya tafiti kwenye madini, Gesi ya Helium ambapo utafiti huo umeibua maeneo mapya kwenye ukanda wa kaskazini tofauti na ilivyozoeleka kuwa helium hupatika maeneo ya kusini. Kwa mujibu wa taarifa za kitafiti za gesi hiyo, Tanzania ina kiasi cha futi za ujazo bilioni 54 za gesi hiyo ambacho kinaizidi nchi ya Marekani yenye hazina ya futi za ujazo bilioni 24.2.
#Aidha, katika juhudi za kuinua Sekta ya Kilimo nchini, GST imefanikiwa kuandaa Ramani inayoonesha viwango vya ubora wa PH (pH values) kwenye udongo, ramani inayohusisha maeneo ya nchi nzima imechorwa/imetengenezwa. Ramani hiyo inaonesha maeneo yenye PH ndogo na kubwa. Pamoja na hayo, GST imewasogezea huduma za maabara wachimbaji wadogo kwa kufungua ofisi ndogo katika maeneo zinakofanyika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini kwa wingi, hivi karibuni tumeshuhudia ufunguzi wa ofisi ya GST mkoani Geita.
# Wizara kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa madini ilianzisha mfuko wa kusomesha wanafunzi wa kike ambapo kwa mara ya kwanza Mwaka 2014 jumla ya wanafunzi 15 walidahiliwa kusoma lapidary. Serikali iliendelea na jitihada za kuzalisha wataalam wa ndani kwa kuleta mtaalam mwelezi kutoa mafunzo hayo kutoka nje ya nchi ikiwemo kuwapeleka wataalam katika nchi mbalimbali kujifunza masuala hayo. Tangu kuanza kutolewa mafunzo hayo, jumla ya wanafunzi 221 wamehitimu mafunzo katika chuo hicho na 117 wanaendelea kupata mafunzo.
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI NA WIZARA YA MADINI