Waziri Biteko hongera kwa kazi nzuri, lakini bado una haya ya kufanya

Waziri Biteko hongera kwa kazi nzuri, lakini bado una haya ya kufanya

Mathanzua

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
17,251
Reaction score
22,929
Waziri Biteko hongera kwa kazi nzuri,ingawa sioni kwamba ni sawa hasa kukupongeza kwa kazi ambayo ni wajibu wako kama Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Hata hivyo nimekupongeza kwa kuwa umethubutu kuvunja upigaji na uzembe ambao ulikuwa umekithiri TANESCO.Sisi wengine tulijua kwamba sababu zote zilizokuwa zinatolewa na Makamba na washirika wake wa upigaji, zilikuwa si za kweli na walikuwa wanatetea tu maslahi yao binafsi.

Sasa tatizo la umeme likiwa nyuma yetu na tukiamini kwamba litakuwa historia,naomba sasa utupie macho maswala ya fuatayo:

1. Ni jambo lililo wazi kwamba wakati uhujumu huo ukiendelea,wananchi tulio wengi vifaa vyetu vingi vya majumbani,hospitalini,kwenye biashara mbalimbali na hata nyumba ziliungua.Kwa bahati mbaya nchi yetu aidha haina Sheria madhubuti za kuwa-compesate wateja wa TANESCO vifaa vyao vinapoungua kwa sababu ya matatizo ya mfumo wa umeme au ni tatizo lile lile la kuendeleza mfumo wa dhuluma na labda upigaji .Haya ni mapungufu makubwa.Naamini ni muda muafaka sasa wa kuwa na Sheria madhubuti za kuwalinda wateja ili TANESCO iwajibike kisheria kuwafidia pindi wanapopata matatizo ambayo yana sababishwa na hitilafu za mfumo wa umeme.

2. Ni muda mrefu tumekuwa na tatizo la umeme,na wengi wetu tulihoji kama kweli tunao ungozi unao wajali wananchi wake,kwa kuwa TANESCO walikuwa wanafanya kazi kama walivyotaka.Kiukweli ni kama hapakuwa na uongozi.Ukatikaji wa umeme ulikuwa wakushangaza,na wala hapakuwa na juhudi zozote za dhati za kuelezea kwa nini tatizo la umeme lipo na kwa nini umeme unakatika katika mfumo unaokatika.Sisi wengine tulibaki midomo wazi kwa mshangao,huku tukijiuliza,viongozi wetu wako wapi?

Jambo lingine la msingi ambalo Waziri Biteko tungetaka ufanye, ni kuwawajibisha wale wote ambao wali sabibishia Watanzania adha ya umeme kwa muda mrefu kiasi hicho,bila kujali athari ambazo wangepata.Ule ulikuwa ni unyama mkubwa sana.Waziri kama utafanya hivyo,utakuwa umewatendea haki Watanzania na kuonyesha kwamba kila tendo ovu lina adhabu na hakuna mtu aliyeko juu ya sheria.Hii itathibitisha kwamba nchi yetu inaongozwa kwa mfumo wa sheria.

3. Bei ya umeme bado ni kubwa sana. Ukizingatia kwamba umeme wa maji ni rahisi kuliko vyanzo vingine vyote,na Hayati Magufuli aliahidi kwamba bwawa la Nyerere litasaidia kushusha bei ya umeme nchi,tunaomba bei za umeme ziangaliwe,upya kwa nia ya kuzipunguza.

4. TANESCO ipate watu wenye weledi wa kutosha na usimazi uwe madhubuti,ili kukwepa ubabaishaji,wizi na ufedhuli kama awali.
 
Mvua zimekata wanakata kata umeme
 
Umeme bei juu bado na sio wauhakika.
Ni sawa mkuu bei ni kubwa bado na tungependa bei ipungue kwa kuwa umeme wa maji ni rahisi zaidi.Kwa kuwa wanapokezana vijiti na Hayati Magufuli aliahidi,hawana budi kutekeleza maono yake..
 
Yaani una maana kwamba kwa sababu mvua zimekata hawapaswi kukata kata umeme? Kama maana yako ndio hiyo, ni kwamba walikuwa wanakati umeme si kwa sababu ya mvua,ila Ilikuwa uhujumu tu kwa taifa na wananchi na upigaji
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom