JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Hatua hiyo inafuatiwa na tukio la hivi karibuni la tembo kuwepo katika eneo hilo na kusababisha taharuki kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara leo Oktoba 28,2024 kwenye Kijiji cha Mkiwa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Mhe. Chana amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo inapungua au kumalizika kabisa.
Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji,Wilaya na Mkoa itafanya zoezi la kutambua na kuweka alama katika maeneo ya Korido za wanyamapori (shoroba) na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutoweka shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.
"Baada ya kuzitambua shoroba tunataka kuwepo na shughuli za uhifadhi mfano kuanzisha Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) ili kuendeleza uhifadhi" Mhe. Chana amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Chana amesema Serikali inaenda kuweka mpango wa matumizi bora ya Ardhi ili maeneo ya mifugo, makazi na kilimo yajulikane.
Mhe. Chana ametaja mikakati mingine ya kudhibiti tembo kuwa ni kuwafunga kola maalum kujua uelekeo wa kundi la tembo,kutoa elimu kwa Askari wa Vijiji (VGS) na kufanya sensa ya wanyamapori.
Soma Pia: Waziri Chana: Serikali Itawalinda Wananchi dhidi ya Wanyamapori wakali
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amewataka wananchi wa Ikungi kutoa ushirikiano kwa Askari Uhifadhi hao ili kukabiliana na tembo ipasavyo.
Mkutano huo umehudhuriwa na wananchi pamoja na Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka Mkoa wa Singida na Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.
Na Happiness Shayo -Ikungi