Waziri Chana: TAWIRI ni moyo wa uhifadhi wa wanyamapori nchini

Waziri Chana: TAWIRI ni moyo wa uhifadhi wa wanyamapori nchini

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana(Mb) amesema Serikali imekuwa ikitumia takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa Wanyamapori ili kuwa na Utalii endelevu.

Mhe.Chana ametoa kauli hiyo leo Oktoba 16,2024 Jijini Arusha wakati akizungumza na Menejimenti yaTaasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro - Arusha ambapo amesema Taasisi hiyo ni muhimu kwa uhifadhi nchini.

" Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi amesisitiza Waziri Chana.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt.Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi Utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza namna bora ya kufanya Utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi.

Soma Pia: Waziri Pindi Chana amezindua rasmi zoezi la Sensa ya Wanyamapori

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt. Thereza Mugobi, wawakilishi kutoka Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Waandamizi kutoka TAWIRI.
IMG-20241016-WA0135.jpg
IMG-20241016-WA0131.jpg
IMG-20241016-WA0132.jpg
IMG-20241016-WA0133.jpg
IMG-20241016-WA0134.jpg
 
Back
Top Bottom