Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Julai 9, 2024 ameanza rasmi ziara katika jimbo hilo kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndumbaro ameambatana na wataalamu mbalimbali kutoka katika Manispaa ya Songea Mjini ili kusikiliza hoja na kero mbalimbali na Kisha kutoa majibu ya kero zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo
Moja kati ya changamoto zilizoibuliwa katika ziara hiyo ni ukosefu wa maji wa muda mrefu katika mitaa ya kata ya Mletele ambayo imetokana na kukosekana kwa bomba la kufikisha maji katika mtaa wa Mdundiko hatua iliyomfanya Mhe. Mbunge atatue changamoto hiyo kwa kujitolea kuchangia kiasi cha shilingi Laki Tano ili kukamilisha kiasi kinachotakiwa ili wananchi wapate huduma hiyo.
Aidha Mhe. Ndumbaro amewaahidi wananchi hao kutatua changamoto ya usafiri wa kufika mjini ambao umekua kikwazo katika eneo hilo.