Waziri Dkt. Ndumbaro Awafariji Waathirika wa Mvua Songea

Waziri Dkt. Ndumbaro Awafariji Waathirika wa Mvua Songea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301


WAZIRI wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Songea Mjini, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewatembelea na kuwafariji waathirika wa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo JAnuari 3, 20255 katika Manispaa ya Songea Mjini mkoani Ruvuma na kuathiri Kaya zaidi ya 50.

Waziri Ndumbaro amewataka waathirika hao kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kutafutia ufumbuzi wa athari hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Wilman Ndile amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wadau wengine inakaa kuona jinsi gani ya kuwasaidia waathirika hao.

Kata zilizoathirika na mvua hizo ni Matogolo (Kaya 340 na Seed Farm (Kaya 23).
 
Back
Top Bottom