Miaka 8 SADC hata ofisi ndogo tu kufacilitate biashara za kimataifa kikanda kutumia uzoefu wake hayo alikuwa anasimamia hana! matokeo anahangaika kutafuta hifadhi kwa watu aliowaacha kijijini kipindi kirefu, leo kawakumbuka kuwa ni wa muhimu..atawafaa nini mtu kama huyu, hata hao ccm kutanguliza mtu wa aina hii ni kama hawawatakii mema watu wa magu!DKT. STERGOMENA TAX ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA SIASA WILAYA MAGU
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Juni 29, 2024 ameungana na Wajumbe wengine kushiriki katika Kikao cha Kamati ya Siasa Wilaya Magu, jijini Mwanza. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za CCM, Magu kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Komredi Enosy Ndobheji Kalambo.
Kuna mahali pameandikwa "Mbunge wa Magu"? Binafsi sijapaona.Kwa hiyo ubunge wa viti maalumu haumtoshi anataka kwenda kugombea Magu.
Tokea lini yeye ni mbunge wa Magu?