Waziri Dorothy Gwajima, ingilia kati harakati za Mwenyekiti wa SUMAUJATA Wilaya ya Moshi Vijijini mtoto huyu apate haki ya elimu

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Ninaandika barua hii nikibubujikwa na Machozi Mimi kama Mzazi lakini nasitika kuona vyombo vya Dola ikiwemo ofisi ya mkurugenzi, wilaya Moshi vijijini, Mkuu wa Wilaya kutotimiza wajibu wao ipasavyo kuhakikisha Vitendo vya ukatili kwa watoto hasa wa kike na kiume havikomeshwi mkoani Kilimanjaro hasa wilaya ya Moshi vijijini

STORY KAMILI IKO HIVI
Mnamo wiki takriban zilizopita, katibu WA SUMAUJATA wilaya ya Moshi vijijini(jina kampuni), alipokea taarifa ya uwepo wa mtoto wa kike anayehisiwa kuwa na umri usiopungua miaka Tisa ya kuwa anatumikishwa na mwanamke mmoja maeneo ya Mbokomu

Baada ya kupata taarifa hizo kupitia ofisi ya Mwenyekiti wa kijiji, katibu aliwasilisha taarifa hiyo Kwa Mwenyekiti wake wa Ulaya ambae nae hakutaka kutajwa jina lake hapa, ndipo wakaanza uchunguzi, katika uchunguzi walibaini ni kweli mtoto huyo aliyetambulika Kwa jina la Diana Emanuel, alikuwa kwa mama huyo akitumikishwa kwa kufanya kazi za ndani, Ili hali alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ambayo haikujulikana kwa haraka Mkoani Kigoma Wilaya ya Kasulu.

Baada ya uchunguzi, Mwenyekiti pamoja katibu wake wakishirikiana na Sumaujata wengine, walifungua shauri kwa ofisi ya Mtendaji wa kijiji, aliyemtorosha na kumtumikisha aliitwa ofisi ya Kijiji na kukiri kufanya kosa ilo na ukatili kwa mtoto huyo huku akidai alimleta Ili ampeleke shule lakini baadae alimgomea na kuanza kumtumikisha kwa kumfanyisha kazi nzito za ndani.

Katika maelezo ya Mwenyekiti wa kijiji alikiri kulijua tukio ilo na kudai ya kuwa si mara ya kwanza kwa Mama huyo kuwafanyisha kazi ndani watoto wadogo na imekuwa ni kawaida yake.

'' Huyu mama Huwa ndo Tabia zake hizi miaka miwili iliyopita kuna mtoto alikuwa anafanya kazi alikuwa mdogo na badala yake yule binti' alitiwa Mimba na mwanae kisha wakamfukuza yule binti' akitoka humu ndani na mimba na hatujui aliko mpaka leo ndio maana huyu mtoto tulilazimika kumripoti Ili kukomesha tabia hizi za ukatili."

KATIKA shauri hilo mwenyekiti wa SUMAUJATa kwa kushirikiana na Mtendaji wa Kijiji walifkia uamuzi mtoto huyo arudishwe Kijijini, kwa gharama za aliyemtorosha,

ALIYEMTOROSHA AGOMA KUMWACHIA MTOTO

Katika hali hisiyotarajiwa mwanamke huyo aligoma kutafuta nauli ya kumsafirisha mtoto mpaka mkoani Kigoma Ili mtoto aweze endelea na masomo

SUMAUJATA wakubaliana kumfikisha mama aliyefanya ukatili Dawati KATIKA kituo Cha polisi Moshi mjini

Katika hali isiyotarajiwa na kushangaza wengi Mwenyekiti wa SUMAUJATa Wilaya ya Moshi Vijijini aliamua kufikisha suala hili Dawati Ili kupata msaada wa kumnusuru mtoto huyo baada ya Ustawi wa Jamii wilaya ya Moshi kushindwa kutoa maamuzi stahiki kwa mtoto, wakiwa kituo cha polisi mama aliyefanya ukatili aliitwa na kukiri kufanya kosa hilo na sasa yupo tayari kumwachia mtoto huyo arudi shule.

Wakiwa Dawati la polisi, Dawati laamua mtoto achukuliwe na Mtendaji wa Kijiji cha Mbokomu huku mama akitafuta nauli ya kumrudisha mtoto Kigoma

Changamoto ilitokea baada ya mtoto kukabidhiwa kwa Mtendaji wa Kijiji nae sasa akaanza kumtumikisha kwa kumgeuza muuza mbege na kumfanyisha kazi za ndani.

'' Akiongea kwa uchungu, moja wa vijana ambae alikuwa na team ya Sumauja wilaya ya Moshi vijijini waliompambania mtoto huyo alisikitika sana kuona ya kuwa wao kwa wao wameanza kugawanyika kwa baadhi kukubali mtoto huyo abakie kwa Afisa Mtendaji wa kijiii cha Mbokumu kwa kumtumikisha kuuza Mbege na kufanya kazi nyingine.

"Huwezi amini yule katibu wetu, ameishatugeuka hayupo na sisi tena anataka mtoto abakie kwa huyo Mtendaji aendelee kutumikishwa sijui amepewa rushwa jaman hii nchi sijui inaelekea wapi jamani?yaani sisi tumechoka lakini tutapambana mpaka tone la mwisho"aliongezea kijana ambaye hakutaka jina lake litajwe mahala hapa.

NAULI YAPATIKANA

Baada ya kuhangaika huku na kule yule mama aliuyemuiba yule mtoto alipata nauli yaa kumsafirisha mtoto yule kupitia Dawati, SuMaujata wilaya ya Moshi vijijini mpaka Arusha Ili aweze kusafirishwa kurudishwa Kigoma kwa lengo la kuendelea na Masomo.

Safari ya kwenda Arusha Ili apakiwe kwenda kigoma yaanza

Pamoja na kupambana Kwa Hawa vijana ambao walijitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanakomesha ukatili huo, hakuna idara ya ustawi wa jamii ambayo ipo chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri iliambatana na msafara wa kumsindikiza mtoto huyo, safari ilianza na hatimaye mtoto alisafirishwa kuelekea Kigoma na amefika huko Leo tarehe 13/10/2022. na kupokelewa na SUMAUJATA wilaya ya Kasulu.

Sumaujata Kigoma apiga simu kwa sumaujata wilaya ya Moshi vijijini alikookolewa huyo mtoto na kuongea mazito huku akitokwa na Machozi dhidi ya jinsi ya kumsaidia mtoto huyo ambaye anaonekana kutelekezwa na wazazi baada ya ndoa kuvunjika

Akiongea kwa uchungu mwenyekiti wa SUMAUJATa wilaya ya Kasulu, alidai hali halisi ya maisha ya mzazi wa yule mtoto ni mbaya sana hana huwezo wa kumsomesha huyo mtoto kwa sababu ni mwanamke hasiye na uwezo na kwa sasa anakabiliwa na jukumu zito la kumlea mtoto wake mwingine ambae ni mlemavu, aliyempata ulemavu baada ya kuwa amemezwa na chatu, na walipomuua chatu mtoto akitoka salama lakini alishikwa na ulemavu ambapo hakai Wala hawezi kula mwenyewe, tukio lililopeleka baba yao kuwafukuza na kutengana na mwanamke huyo jambo linalofanya huyu mama mwanaye ahangaike.

" Dada ungejua Huyu mtoto usingemrudisha angesomea huko kwa msaada wa wasamaria wema kama wapo yaani huku hakuna uwezo, Kabisa yaani Huyu mtoto baba yake ni Mtanzania ila mama yake inaonesha ni Mrundi, alifunga ndoa na mwanaume anaejulikana Kwa jina moja la Emmanuel yeye akitokea kwenye kambi ya wakimbizi ila mwanaume ni mwanajeshi yupo mpaka wa Tanzania na Burundi ni Mwanajeshi wa jeshi la wananchi, ameisha achana na huyu mwanamke mbele ya Mahakama, Sasa Mimi mtoto nimempokea nampeleka kwa mama yake lakini sidhani kama ataweza imiri hizi shida, labda cha kusaidia tutafute mawasiliano na wizara usika iweze ona jinsi ya kumsaidia

"Dada huwezi amini huyu mtoto mtihani wa darasa la nne alikuwa mwanafunzi wa Tisa kati ya wanafunzi zaidi ya mia lakini anakosa fursa ya kupata elimu kisa umasikini na migogoro ya ndoa ya wazazi.

Wito Kwa idara za Serikali, "sisi kama sumaujata hatulipwi chochote, uwezi amini tangu tumeanza kufuatilia Ili jambo tunatumia gharama zetu, ila Kuna watumishi wa umma walioajiriwa ili kupambana ukatili wa namna hii, tunasikitika wanaposhindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo na hata tunapowasaidia wao wanahisi tunataka kuchukua nafasi zao sijui?" Mimi nilifanya hivi Kwa sababu ni mzazi, lakini serikali kupitia watumishi iliyowaajiri ni vyema wakatimiza wajibu wao.

Ombi
Kwanza namwomba Mh DOROTH GWAJIMA kama atapata taarifa hii awasiliane na sisi kupitia namba hii Ili tujue jinsi ya kuweza kumnusuru huyu mtoto ambaye ni Nguvu kazi ya Taifa sisi tupo tayari 0627616227

Mwandishi ni mpita njia tafadhali ni vyema asamehewe kwa jinsi alivyoandika.
 
Huko Moshi punguzeni unywaji wa pombe uliopitiliza.
 
Nadhani huko kigoma kitafutwe kituo cha kumsaidia huyo mtoto ingesaidia zaidi

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom