Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt . Dorothy Gwajima ameeleza kusikitishwa na tukio linalodaiwa kufanywa na mkuu wa wilaya ya Songwe, Simon Simalenga la kumpiga na kumjeruhi binti mwenye umri wa miaka 20 Florenencia Mjenda, mkazi wa kata ya Mbangalo wilayani humo.
Dkt. Gwajima amesema tukio hilo ni la kweli kama lilivyoripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na tayari binti huyo amefungua kesi polisi ya shambulio la aibu katika kituo cha Mkwajuni.
Waziri Gwajima amesema ametuma kikosi cha maafisa ustawi wa jamii kwenda nyumbani kwa binti huyo, ili wampe ushauri nasihi wakati shauri hilo likiendelea na amewataka wasaidizi wa kisheria wafuatilie kwa karibu hatua zote.
Ametoa wito kwa viongozi kuacha kwenda nje ya taratibu na kuanza ugomvi binafsi na wananchi ambapo wanawake, wasichana na watoto wanakuwa waathirika.