mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa jamii kuwapa wanawake nafasi na sauti katika uongozi, akisema kuwa bila juhudi za makusudi za kuwaunga mkono, usawa wa kijinsia hautafikiwa.
Waziri Gwajima ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, Februari 11, 2025 alipohutubia kama mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Programu ya Uongozi wa Wanawake Vijana (Young Women Leadership Program - WYLP) inayoratibiwa na Care International Tanzania kwa kushirikiana na Mwanamke Initiatives Foundation.
Soma Pia: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Mwanamke Initiatives Foundation, Wanu Hafidh, ameeleza kuwa yeye mwenyewe ni mnufaika wa programu za uongozi na anafahamu umuhimu wake kwa wanawake vijana, hivyo anaamini kuwa programu hiyo itatoa mafunzo ya uongozi, ushawishi na utetezi wa haki za wanawake, hivyo kuwawezesha wanawake vijana kushika nafasi mbalimbali za maamuzi.
Naye Mkufunzi wa programu hiyo Imani Kajula amesema kuwa ana imani wanawake hao watajifunza masuala mengi yanayohusu uongozi na kuongeza idadi kubwa ya viongozi wanawake katika jamii lengo likiwa ni kupunguza pengo lililopo kati ya wanaume na wanawake katika uongozi.
"Baada ya kuhitimu mafunzo kama haya, hatua inayofuata ni utekelezaji wa yale tuliyojifunza ili kuleta mabadiliko. Uzinduzi wa WYLP ni sehemu ya kuandaa viongozi wa baadaye ambao watakuwa na mchango mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla," amesema.