#COVID19 Waziri Gwajima: Mikoa itakayozembea kuchanja Corona itanyang'anywa chanjo na kupelekewa mikoa iliyochangamka

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa afya Dkt. Gwajima amesema mikoa itakayoonyesha kusuasua kwenye uchanjaji wa Corona basi watanyang'anywa hizo chanjo na kupelekewa mikoa iliyochangamka katika uchanjaji.

Chanzo: Star tv habari

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Marekani raisi Biden kaomba kuwa iidhinishwe watu wapewe dola 100 Kila mmoja atakayetaka chanjo ili wachangamkie chanjo baada ya kuona watu wa chini wamegoma kuchanja na wanalia Hali ngumu ya maisha kutokana na measures za Vita dhidi ya corona
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Pale ambapo Mawaziri na Serikali ya Muhula wa 6 inapogeuka kuwa maofisa masoko wa kampuni ya JJ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hawa wamesema Kilimanjaro na Arusha hali ni Mbaya kwa nini wasichukue hz chanjo milion 1 wakawape wachaga huko Kilimanjaro na Arusha ??
 
Yuko sahihi.

Mh.Rais ameshafafanua.

Waziri wa afya ameshafafanua.

Kipi kingine?

Kwa kuwa ni HIYARI....tutachanja tunaokubali.

#NajiandaaKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Waziri wa afya Dkt. Gwajima amesema mikoa itakayoonyesha kusuasua kwenye uchanjaji wa Corona basi watanyang'anywa hizo chanjo na kupelekewa mikoa iliyochangamka katika uchanjaji.

Chanzo: Star tv habari

Mungu ni mwema wakati wote!
Anawaadhibu wananchi kwa sababu ya uzembe wa watendaji? Au kusuasua anakomaanisha ni watu kutojitokeza? Kama ni hivyo, ni busara kufanya hivyo maana chanjo zina expiry date.

Amandla...
 
Wachaga wanachanja Astra hapo kwa Uhuru bwashee!
 
Ni Gwajima yuleyule aliekuwa anahubiri kujifukizia na kupinga chanjo au ni Gwajima mwingine?Kama ni Gwajima yule yule mwambie kuwa sisi mkoani kwetu hatutaki chanjo, tumechagua kujifukizia.
 
... mdogo mdogo chanjo inaelekea kuwa mandatory for every citizen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…