Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Wewe waziri wa afya kama daktari msomi mpaka leo dunia nzima ilikushangaa sana pale ulipokaa mbele ya kamera za wanahabari ukajifukiza na kisha kunywa mchanganyiko wa malimao, tangawizi na pilipili na kuwaaminisha Watanzania kuwa hiyo ni kinga na tiba ya Uviko-19.
Limekuja suala la chanjo ya uviko kutumika hapa nchini unatumia nguvu nyingi sana kutaka watu wachanje. Hilo ni jambo jema. Lakini kama mtaalamu tuambie watanzania hii chanjo ya Johson and Johnson inafanya kazi vipi na ina kinga mwili vipi dhidi ya Uviko -19 kuliko kutishia watu wanaohoji vituko vyako.
Ulipojifukiza na kunywa Bupeji watu walihoji usomi wako. Maana virus wa Uviko-19 akishaingia kwenye mapafu kumtibu kwa malimao na mvuke ni ngumu. Lakini ulikoamalia mvuke na Bupeji. Watu wanahoji juu ya hizi chanjo, unaropoka kuwa hazimalizi nguvu za kiume. Mume wako amechanja na anapiga kama kawa.
Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Hakuna haja ya kutisha watu wanapohoji vituko vyako. Watanzania wanahitaji maelezo ya namna hii chanjo inamkinga mtu dhidi ya Uviko-19.