#COVID19 Waziri Gwajima, tumia busara na elimu yako kuinadi chanjo ya UVIKO -19, usitumie mabavu kama ulivyoinadi nyungu na Bupeji

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Wewe waziri wa afya kama daktari msomi mpaka leo dunia nzima ilikushangaa sana pale ulipokaa mbele ya kamera za wanahabari ukajifukiza na kisha kunywa mchanganyiko wa malimao, tangawizi na pilipili na kuwaaminisha Watanzania kuwa hiyo ni kinga na tiba ya Uviko-19.

Limekuja suala la chanjo ya uviko kutumika hapa nchini unatumia nguvu nyingi sana kutaka watu wachanje. Hilo ni jambo jema. Lakini kama mtaalamu tuambie watanzania hii chanjo ya Johson and Johnson inafanya kazi vipi na ina kinga mwili vipi dhidi ya Uviko -19 kuliko kutishia watu wanaohoji vituko vyako.

Ulipojifukiza na kunywa Bupeji watu walihoji usomi wako. Maana virus wa Uviko-19 akishaingia kwenye mapafu kumtibu kwa malimao na mvuke ni ngumu. Lakini ulikoamalia mvuke na Bupeji. Watu wanahoji juu ya hizi chanjo, unaropoka kuwa hazimalizi nguvu za kiume. Mume wako amechanja na anapiga kama kawa.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Hakuna haja ya kutisha watu wanapohoji vituko vyako. Watanzania wanahitaji maelezo ya namna hii chanjo inamkinga mtu dhidi ya Uviko-19.
 
Wewe waziri wa afya kama daktari msomi mpaka leo dunia nzima ilikushangaa sana pale ulipokaa mbele ya kamera za wanahabari ukajifukiza na kisha kunywa mchanganyiko wa malimao,tangawizi na pilipili na kuwaaminisha watanzania kuwa hiyo ni kinga na tiba ya Uviko-19
Your browser is not able to display this video.
 
Mabavu aliyotumia waziri ni yapi? kusema Gwajima askofu athibitishe tuhuma dhidi ya Rais kula hongo?

Nimemsikia waziri akizungumza mambo kisayansi mara nyingi tu, ndio maana anamtaka Gwajima asie mwanasayansi athibitishe madai yake.

Habari ya nyungu kwa sasa ilishapita, kama mamlaka ya uteuzi iliamua kuwaacha mawaziri wa mwendazake sioni sababu kumpigia kelele huyo mama.

Hata Gwajima msanii nae alituambia Corona haitaingia Tanzania, but leo anaruka ruka hataki kuchanjwa, hayo maombi yake kama hayakuizuia Corona kuingia Tanzania, kwanini leo aaminiwe yatawakinga watu wasipate Corona?
 
 

Attachments

  • IMG_3934.MP4
    1.7 MB
Waziri Gwajima hana credibility tena ya kuaminiwa ktk muktadha huu wa COVID, mtu yule yule hawezi kuwa hasi na chanya ktk jambo moja.

WATANZANIA SIO WAJINGA KIASI CHA KUSHINDWA KUHOJI VITU VYA MSINGI
 
Hata aje nani kunadi there's no way mamillion ya watu watachanja, labda wazee na watu wanaoona they have nothing to loose. Hii nchi ni ya vijana kwa mamillion, kuwapata hao ni sawa sawa na kutembea juu ya jua. People are not as stupid as you think.

Kama survive late ya Covid 19 kwa vijana ni zaidi ya 97% bora nipate hiyo covid mwili wangu utatengeneza antibodies, a natural immune sio sindano sijui content yake ni nini.
 
Sasa Mshana Jr ndio umepost nini? Naona kama umeirudia tu sehemu ya post ya mtoa mada
 
Ndugu yangu. Madakatari wenyewe wanahimisa milo safi na yenye vitamin na kujenga mwili. Wakikupa dawa za hospital wanakuongezea na milo
 
Ndugu yangu chagu mara nyingi imesemwa tutafika mahali tutaongea lugha moja,tayari nawe uummoja wao,ni hatua njema kwa anayejifunza na kutambua alikosea wapi,huyo sikuzote huwa mwalimu mnzuri,tukumbuke siasa ni siasa na maslahi ya taifa ni zaidi ya siasa..
 
Na leo amebadilika, sijui tumweleweje.
 
Anasema kuwa eti mchakato wa chanjo aliuanzishaga magufuli hivyo samia anatekeleza tu.

Hivi DOROTHY anatuona ni watu wenye AKILI NDOGO KAMA YAKE.
 
Unategemea mtu kama huyu awe na moral authority ya kunadi chanjo?🤡🤡🤡
Your browser is not able to display this video.
 

Hii ndio shida ya kujitoa fahamu na kuchanganya siasa na sayansi kinafiki kumuunga mkono Mwendazake. Sasa hayupo wote wanapambana na mauza uza yake. Bahati nzuri uongozi mzima ni ule ule sasa watuambie nini haswa wanaamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…