figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Waziri wa afya Dr. Hussen, amewataka waganga wa kienyeji wapeleke dawa zao NIMR ili zichunguzwe kama hazina madhara. "Hizi dawa za kienyeji zimekuwa zikisaidia sana watanzania, sasa imefikia wakati wa dawa hizi kupelekwa nimr ili zifanyiwe uhakiki kama hazina madhara. wapo ambao wameshaanza kupeleka dawa nimr.MY VIEW;Kipindi cha nyuma kuna waziri alipiga marufuku waganga wa kienyeji na kuagiza wafutiwe leseni. Imekuaje sasa? serikali imeshindwa kununua dawa za kuwahudumia watanzania?Ikoje hii?. mia
Unajuan sometime kama hujawa covered kwa muda mrefu na vyombo vya habari ndo madhara yake haya.
Kuna wakati Tanzania walipiga marufuku kuvaa vi mini na suruali zilizobana. Mbona sasa zinavaliwa? Ikoje hiyo?
Duh?!..Sijaelewa halisi, katika medicine kuna kitu kinaitwa Alternative medicine, which is partially acceptable, swali langu ni vipi je ndiyo hii au wanataka ile ya Traditional healer"wapiga ramli" ndio ihalalishwe?..msaada wakuu.
Hakuna waziri aliyewahi kupiga marufuku waganga wa kienyeji Tanzania. Kinachofanyika siku zote ni kuwahamasisha wafuate taratibu za kujisajiri ili watambulike rasmi...
Ni Pinda alietoa kauli ya kufuta leseni za waganga wa kienyeji,ni baada ya kukithiri kwa mauaji ya maalbino nchini. Hatua iliyofikia Pm.Pinda kulia bungeni.!
Can you give a quote?
yeye kazungumzia dawa za kienyeji zote zipelekwe nimr. mia